Ilikuwa
tarehe kama ya leo miaka 23 iliyopita wakati ndege iliyokuwa imebeba
wachezaji 18 wa kikosi cha timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo , watu wa
nne wa benchi la ufundi akiwepo kocha mkuu wa timu hiyo Godfrey Ucar
Chitalu na wasaidizi wake watatu , na viongozi watatu wa chama cha soka
cha Zambia ilipopata ajali mbaya kwenyenpwani ya Gabon na kuua watu wote
30 waliokuwemo .
Ndege
hiyo aina ya DHC-5D Buffalo ikiwa na namba za usajili (AF-319)
ilianguka na kuzama kwenye bahari ya Atlantic karibu kabisa na pwani ya
mji mkuu wa Gabon Libreville baada ya matatizo ya kiufundi . Kwa mujibu
wa uchunguzi uliofanywa na jeshi la Gabon ndege hiyo ilipata hitilafu
iliyosababisha moto kwenye moja ya Injini zake hali iliyomlazimu rubani
Kanali Fenton Mhone kuizima injini hiyo , hata hivyo Rubani alikosea na
kuzima injini nyingine iliyokuwa nzima hali iliyofanya ndege hiyo
kushindwa kwenda vizuri na hatimaye kuanguka baharini .
Zambia
ilikuwa njiani kuelekea Senegal ilikokuwa inaenda kucheza na timu ya
taifa hilo katika michezo ya hatua za mwisho ya kufuzu kucheza kombe la
dunia mwaka 1994 huko Marekani .
Moja
ya watu waliosalimika kwenye ajali hiyo alikuwa nyota wa enzi hizo wa
timu ya taifaya Zambia Kalusha Bwalya ambaye hii leo ni Rais wa chama
cha soka cha Zambia FAZ ambaye alichelewa safari hiyo abapo alikuwa
anatokea nchini Uholamzi alikokuwa anacheza soka la kulipwa .
Ajali
hii ndio ajali mbaya kuliko zote kwneye historia ya soka la Zambia na
iliilazimu nchi hiyo kuunda timu mpya kwa haraka ambayo iliongozwa na
Kalusha Bwalya.
Cha
kushangaza ni kwamba timu mpya iliyoundwa kwa haraka haraka iliweza
kufuzu kucheza kombe la mataifaya Afrika mwaka uliofuatia ambapo ilifika
fainali ilikofungwa na Nigeria 2-1.
Hadi
leo kikosi hicho ambacho kilikuwa na wachezaji maarufu kama Kipa Efford
Chabala , beki Eston Mulenga ,kiungo Moses Chikwalakwala na
mshambuliaji Patrick ‘The Bomber Banda kinaaminika kuwa kikosi bora
kilichowahi kutokea kwenye soka la Zambia na wengi walitarajia kukiona
kiiwakilisha Afrika kwenye fainali za kombe la dunia Maka 1994.
Kocha
wa timu hiyo Godfrey Ucar Chitalu alipata umaarufu mkubwa enzi zake
akiwa mshambuliaji wa klabu ya Kabwe Warriors ambapo aliwahi kuweka
rekodi a kufunga mabao 117 kwenye msimu wa mwaka 1972 rekodi ambayo FIFA
imegoma kuitambua . Rekodi hiyo ilitajwa san