Sasa unaweza kuacha urithi wa vitu unavyomiliki mtandaoni kutoka Google.
Mfano kama una blog ( kupitia Blogger), una picha (zilizopo kwa Picasa
Web Albums), na documents mbalimbali zilizopo kwa Google Drive, unaweza
kuigiza Google kuwa endapo utafariki, vitu vyako hivyo vikabidhiwe kwa
mtu fulani.
Tunapozungumzia kufariki ni kuwa Google haitojua kuwa umefariki au la,
ila kutokana na kutokutumia kwako kwa muda mrefu akaunti yako ya Gmail,
na kwa maagizo utakayokuwa umeacha kuwa endapo itatokea haujaitumia kwa
muda mrefu basi Google itume kazi zako kwa huyo utakayeamua atumiwe.
Huduma hii maalum iitwayo Inactive Account Manager,
inaweza pia kunufaisha hata pale mtu anapokuwa amepelekwa jela kwa muda
mrefu, au ameamua kuacha kutumia huduma za Gmail, hivyo kuamua kufunga
akaunti yake na huduma nyinginezo toka Google.
Unachotakiwa kufanya ili kuagiza Google waigawe akaunti yako, na vitu vyako vingine, fuata hatua hizi:
1. Nenda kwa ukurasa wa huduma hii Bofya hapa (Inactive Account Manager)
2. Kisha jaza hatua kwa hatua mambo taarifa ambazo Google wanataka toka kwako. Taarifa hizo ni :-
Alert Me : Hapa utajaza namba ya simu na email address nyingine
ambapo Google watafanya jitihada za kukutaarifu kuhusu kutaka kwao
kufunga au kugawa akaunti yako.
Time out period: Hapa utajaza muda ambao unataka Google wasubiri
kama upo kimya kutumia akaunti yako. Muda huu ndio utakaowawezesha
kujua kama kweli wewe ni mtumiaji hai au la. Na mara baada ya muda huu
kupita, basi Google watajaribu kukuandikia email kwa anuani nyingine
uliyojaza au kukutumia SMS kwa namba utakayokuwa umeijaza katika
kipengele cha Alert Me.
Notify contact and Share Data: Hii ni sehemu muhimu ambapo Google
itagawa taarifa zako kwa mtu au watu utakaoagiza. Pia watu waweza
kuagiza watu hawa wapewe taarifa. Na kama upo hai au unaweza bado
kutumia email yako, basi watu hao watakuuliza wewe kabla ya kukubali
kupokea taarifa zako.
Optionally delete account: Hiki ni kipengele ambapo unaagiza
Google waifute akaunti yako baada ya muda ulioujaza katika kipengele cha
Time Out Period, kupita.
3. Ukisha jaza vipengele vilivyotajwa hapo juu, unabofya Enable, ili uanze kuitumia huduma hiyo.