Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, April 29, 2013

BREAKING NEWZZZ ..... MH. GODBLESS LEMA AACHIWA HURU KWA DHAMANA ..... ONA MATUKIO YALIVYOKUWA HATUA KWA HATUA


MH. LEMA AKIWA KIZIMBANI
 
***********
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema, leo amepandishwa kizimbani jijini Arusha na kusomewa shitaka lililokuwa likimkabili na kuachiwa kwa dhamana iliyokuwa na masharti rahisi.

Godless Lema, alikuwa akishikiliwa na polisi mkoani humo kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu zilizosababishwa na wanafunzi kwenye chuo cha Uhasibu mwanzoni mwa wiki iliyopita mwenzao kuuwawa huko maeneo ya njiro jijini humo.

Mbunge huyo alikamatwa siku ya Ijumaa na kuwekwa rumande kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa wa Arusha, Magesa Mulongo.

Baada ya kuachiwa mahakamani hapo mbunge huyo ameongozana na wafuasi wake kwa msafara wa maandamano na mapikipiki kuelekea katika Ofisi za Chama hicho.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...