Machinga wakiendelea na shughuli zao kama kawaida eneo la mashine Tatu asubuhi hii kutokana na kauli ya mbunge Msigwa kuwaruhusu kurejea ,chini polisi wakiwa eneo hilo |
Hali si shwari
katika Manispaa ya Iringa baada ya kauli mbunge wa jimbo hilo
Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kuwataka wafanyabiashara wadogo wadogo
(machinga) kurejea kufanya kazi katika eneo la barabara ya
Mashine tatu kutekelezwa na machinga hao.
Msigwa
ambae aliitoa kauli hiyo April 23 mwaka huu katika mkutano wa wabunge
wa chadema waliosimamishwa bungeni ,mkutano uliofanyika
katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa,kwa kuwataka
Machinga kurejea eneo hilo na iwapo mtu atafika kuwanyanyasa basi
wana----!!!?
Machinga hao leo wameitikia
kauli hiyo kwa kurejea eneo hilo na kupelekea askari wa kutuliza
ghasia (FFU) kutanda eneo hilo na kushindwa kutumia nguvu zaidi
ya kuwataka wafanyaiashara hao kuendelea na shughuli zao eneo hilo .