Askofu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Alex Malasusa, jana Aprili
15, 2013 amechangisha zaidi ya Milioni 64/- katika Harambee ya Ujenzi wa Kanisa
la Usharika wa Mpwapwa, ambapo WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel
Sitta, alinunua Tenga la Kuku kwa Shilingi Milioni Moja.
Sitta akiwa
miongoni mwa wabunge waliopigiwa simu na Askofu Dkt. Malasusa ili kuwajulia hali
kutokana na majukumu ya kitaifa ya Bunge waliyonayo mjini Dodoma, aliitikia wito
wa Baba Askofu Malasusa na akamuunga mkono kwa kununua Tenga la Kuku kwa Milioni
Moja Taslimu.
Aidha
Katika changizo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Christopher Kangoye alichangia
Shilingi Milioni 1.5/-, katika Harambee hiyo ambayo Askofu Malasusa pamoja na
mambo mengine alichangisha zaidi ya Milioni 64/=.
Kwa upande
wa waumini kila aliyechangia Harambe na kutaka kupiga picha na Mkuu wa KKKT
Askofu Malasusa, alijikuta akifunguliwa mioyo na
kupiga naye picha Moja kwa Shilingi Laki 5/-, tofauti mahali pengine ambapo
hupiga naye picha kwa Shilingi 50/-.
Tunu na
Baraka ya pekee ilikuwa ni kwa Mtoto aliyebatizwa papo kwa papo, huku wazazi
wake wakiridhia kufunga Harusi (Pingu za Masha) ingawa walipoamka asubuhi
hawakuwa na lengo wala ndoto za kufunga Ndoa siku hiyo.
Kwa muujiza
huo, Askofu Mkuu wa Dayosisi ya KKKT Dodoma Amoni Kinynyu alisema, vyeti vya
wana ndoa hao zitasubiri siku 21 za tangazo la ndoa kuona iwapo kutakuwa zuio
lolote la harusi yao kisheria na zitakapomalizika bila zuio watakabiddhiwa
shahada zao.