Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Showing posts with label afya. Show all posts
Showing posts with label afya. Show all posts

Monday, August 18, 2014

SERIKALI YA ZANZIBAR YATOA TARIFA JUU YA UGONJWA HATARI WA EBOLA.

01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Vuga kuhusu Ugonjwa wa Ebola na mikakati ambayo SMZ inaendelea kuichukuwa ili kukabiliana na ugonjwa huo hatari, hadi sasa hakuna mgonjwa alieyegundulikana na ugonjwa huo Zanzibar.
 02Wandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Waziri Mohammed Aboud alipokuwa akitoa tarifa juu ya ugonjwa hatari wa Ebola Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. 03Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed akifafanua kitu wakati wa Mkuta wake na wanahari. Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.
NA/JAMILA ABDALLA –MAELEZO ZANZIBAR.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  imeanza kuchukua hatua mbali mbali za kukabiliana na Ugonjwa hatari wa Ebola ambao unazidi kusambaa katika nchi mbali mbali Barani Afrika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar kuhusiana na mikakati ambayo SMZ inaichukua ili kukabiliana na ugonjwa huo.
Waziri Aboud amesema licha ya kwamba Zanzibar hakuna Mgonjwa aliyegundulika kuwa na Ebola lakini mazingira yanaonesha kuwa Zanzibar inaweza kupata maradhi hayo kutokana na kuwa na muingiliano mkubwa na nchi nyingine ambazo tayari zimethiriwa na Ugonjwa huo.
Ametaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari juu ya maradhi ya Ebola na namna ya kujikinga.
 Mh: Aboud amesema kuwa pia serikali itaimarisha taratibu za ugunduzi ,ukaguzina ufuatiliaji wa washukiwa wa ugonjwa huu katika bandari ,viwanja vya ndege,vituo vya afya na jamii kiujumla.
Akiendelea kufahamisha mikakati hiyo waziri huyo amesema kuwa Pia serikali imeandaa maeneo maalumu kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa Ebola ambapo wizara ya Afya watayatangaza hivi karibuni.
Pamoja na mikakati hiyo waziri Aboud amewaomba waandishi wa habari kusaidia katika kusambaza elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa huo.
Akitaja dalili za ugonjwa huo Waziri Aboud amesema kuwa dalili kuu ni homa, maumivu makali ya kichwa, misuli na viungo vya mikono na miguu pamoja na koo.
Dalili nyengine ni kukosa nguvu za kiwiliwili na kufuatiwa na vipele katika ngozi,macho kuwa mekundu na kutokwa na damu katika tundu mbalimbali za mwili ikiwemo pua ,masikio mdomo na ngozi.
Kwa upande mwengine waziri ametaja njia zinazotumika kusambaza ugonjwa huo kuwa ni kugusana mojakwa moja na mtu aliyeambukizwa ,kugusa majimaji yanayotokana na mgonjwa kama vile damu,jasho, mate ,mkojo na makohozipamoja na kutumia vifaa vilivyotumiwa na mgonjwa mwenye maambukizi bila kusafisha vizuri.
Read More >>

Friday, January 3, 2014

NHIF yatatizwa na wanachama wadanganyifu


Ukiukwaji wa utaratibu wa kujumuisha wategemezi  wanaostahili kupata huduma za matibabu kupitia Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), unatishia uhai wa mfuko huo ambao hadi sasa umeishafikisha mahakamani kesi zaidi ya 18 katika mahakama 
 

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Hamisi Mdee alisema kuna udanganyifu mkubwa ambao unafanyika katika uandikishaji wa wategemezi wanaostahili huduma za matibabu.

Alisema udanganyifu mkubwa unafanywa na baadhi ya wanachama wa mfuko huo ambao wanauza nafasi za wategemezi wao kwa watu wenya mahitaji makubwa ya matibabu ili kujipatia fedha kinyume cha sheria hususan wale wa magonjwa ya figo na saratani.

Mdee alisema mgonjwa anayehitaji kusafishwa figo mathalani husafishwa mara tatu kwa wiki na inagharimu sh300,000 kwa mara moja kiwango ambacho ni sawa na sh900,000 na upande wa saratani kipimo cha ugonjwa huo (Chemotheraphy) ni  sh1.3 milioni hadi 4 na dozi nzima ni sh24 milioni.

“Watu wanauza majina ya wategemezi wao kwa watu wengine jambo ambalo linautia mfuko hasara na kutishia kuwepo kwake” Mdee alisema na kuongeza kuwa kutokana na hali hiyo mpango huo ni endelevu hivyo hugharimu mfuko fedha nyingi na mbaya zaidi ni kwa watu ambao si walengwa.

Alisema kutokana na kubainika kwa ulgahai na hujuma za namna iyo mfumo hivi sasa umeweka utaratibu wa usajili wa wategemezi wanaolengwa na mfumo ambao ni pamoja na mwenza halali wa mwanachama mchangiaji.

Wengine ni watoto wa kuzaa au kuasili wa mwanachama mchangiaji, wazazi wa mwanachama na au wazazi wa mwenzi wake na kulingana na utaratibu huo kuanzia hivi sasa huduma za matibabu zitatolewa kwa wale tu wenye vitambulisho na sio vinginevyo kulingana na utaratibu wa sasa.

Siku za karibuni kumekuwa na matukio mengi ya watu kukamatwa wakitumia vitambulisho vya watu wengine ili kupata matibabu ya maradhi mbalimbali na maeneo mengine wamekuwa wakipata huduma hizo bila kubainika jambo ambalo linaugharimu mfuko.
Read More >>

Thursday, August 15, 2013

MKUU WA WILAYA YA MAKETE AZINDUA MRADI WA MAPAMBANO YA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI.


Shilika lisilo la kiserikali la support makete  to self support SUMASESU limezindua mradi  wa miaka miwili wa mapambano ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa vijana wenye umri wa kuanzia miaka kumi na tano  hadi ishirini na nne

Akizindua mradi huo mkuu wa wilaya ya Makete Bi Josehine Matilo hapo juzi alisema kuwa kuna vijana wengi mitaani  ambao wanakosa shughuli za kufanya na kuwataka kuunda vikundi vya ujasiliamali kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika sambamba kuvitumia vikundi hivyo katika shughuli za uzalishaji ikwemo kilimo ili kuendana na kauli mbiu ya kilimo kwanza  ikilinganisha na ardhi ya makete kukubali kilimo cha mazao mbalimbali.

Pia bi matilo amewataka viongozi wa ngazi ya kijiji kata hadi wakuu wa idara ikiwa pamoja na idara ya afya  kuonyesha ushirikiano wa kutosha  kwa shirika hilo katika utekelezaji hadi kufikia malengo ya  wa mradi huo na kukiri kuwa kuna baadhi ya miradi imekuwa ikishindwa kumalizika kutokana na miradi hiyo kuachiwa mashirika pekee katika utekelezaji

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika hilo bw.Egnatio Mtawa  amessema kuwa wataweka muda wa kupima utekelezaji wa mradi huo pamoja na uundaji wa vikundi vya vijana na kuwaomba viongozi wa  ngazi mbalimbali hasa maeneo yanayotarajiwa kunufaika na mradi huo kwa kuonyesha ushirikiano kwenye utekelezaji wa mradi huo

naomba niahidi kitu kimoja kwamba tutaweka muda wa kupima utekelezaji wa mradi kwamba siku ile tulielekeana hivi na utekelezaji umafikia na tumekutana na changamoto hiziikiwa pamoja na uundaji wa vikundi naomba na serikali katika baadhi ya sekta hasa watu wa afya alisema bw Mtawa 

Aidha kwa upande wake diwani wa kata ya Iniho ambaye pia ni makamu mwenekiti wa halmashauri ya wilaya Bw Jison Mbalizi alisema kuwa katka kata tano ambazo zinatarajia kunufaika na mradi huo ni zinatakiwa  kiwa mfano wa kuigwa katika mapambano ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na kuahidi kwa upande wake konyesha ushirikiano pindi shirika hilo litakapo wasili katika kata yake

Miongoni mwa kata ambazo zinatarajia kunufaika na mradi huo ni pamoja na Kitulo, Ipelele, Iwawa, Isapulano,na Iniho.
Read More >>

MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA WAVUKA LENGO

 Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Bw. Rajab Mwenda akizungumza na waandishi wa habari jana kutoa takwimu za makusanyo ya damu kwa mwezi Aprili mpaka Juni mwaka huu ambapo ulivuka malengo kwa asilimia 111 kutoka chupa 36,278 mpaka 38,948. Kulia ni Ofisa Msaidizi wa Masoko na Uhusiano Bi. Rayah Hamad  (Picha na Mpiga picha maalum).
                 
 ==== ========   ======
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama umevuka lengo la makusanyo ya damu katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu kwa kukusanya chupa za damu 38,948 ambazo ni asilimia 111 ikilinganishwa na  chupa 36,278 zilizokusanywa kutoka Januari hadi Machi mwaka huu.

Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Damu Salama, Bw. Rajab Mwenda akizungumza jana Dar es Salaam alisema kanda inayongoza kwa uchangiaji ni Mashariki na Kanda ya Ziwa.
Alisema mafanikio hayo yametokana na uanzishajiwa mpango wa damu salama wa  kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu kwa hiari  katika jamii na kushirikisha wadau.

 Bw. Mwenda alisema maadhimisho ya siku ya wachangia Damu duniani ambapo lengo la kukusanya chupa za Damu 8,500 kutoka kanda sita za mpango wa Taifa wa damu salama liliwekwa na mpango ulifanikiwa kukusanya jumla ya chupa 8,683
  
Alisema Mpango wa Damu salama kushirikiana na wadau mbalimbali kama asasi za kiraia nayo imeongeza makusanyo ya damu toka vituo vidogo vya kuchangia damu Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,  Morogoro na Dodoma kutoka chupa za damu 2,560 mpaka chupa3,151 kufikia Aprili hadi Juni mwaka huu.

 Aliwaomba wadau kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari kwa kutumia vyombo vya habari, mitandao ya jamii na vipeperushi.

Bw. Mwenda alisema ushirikiano ni mdogo kati ya wahamasishaji wa Mpango  wa damu salama na viongozi wa Taasisi mbalimbali, matumizi mabaya ya damu kidogo inayopatikana katika hospitali zetu na miundo mbinu hafifu hususan barabara mbovu wakati wa ukusanyaji  na usambazaji wa damu.

Alisema changamoto nyingine ni uuzwaji wa chupa za damu kunakofanywa na baadhi ya watumishi wa hospital ambao si waaminifu hivyo kukatisha tamaa wachangia damu kwa hiari.

Bw. Mwenda alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilianzisha Mpango wa Taifa wa Damu Salama mwaka 2005 ili kuhakikisha uwepo wa damu salama na ya kutosha kwa wote wanaohitaji. 

Alisema shughuli za mpango ni pamoja na uhamasishaji jamii kuhusu uchangiaji damu wa hiari, ukusanyaji upimaji na usambazaji wa damu salama mahospitalini.

“Mpango wa Taifa wa Damu salama unafanya kazi kwa kushirikianana kitengo cha kuzuia magonjwa (CDC)  na wadau wengine wa Chama cha Msalaba Mwekundu na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)” alisema Bw. Mwenda. 

Alisema Mpango wa Taifa wa Damu salama uliweka lengo la kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) katika damu iliyokusanywa asilimia 1.1 kwa kipindi Aprili- Juni ikilinganishwa na asilimia 1.2 kipindi cha Januari hadi Machi baada ya kujikita katika suala la uhamasishaji na kutoa damu toka kwa jamii ambayo ni salama, kuboresha dodoso la wachangiam damu na kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu na wachangiaji kujiepusha na tabia hatarishi ili wawe wachangiaji wa kujirudia.
Read More >>

SERIKALI YAPAIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIK HAPA NCHINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Mamaku wa Rais Mazingira,Dkt. Terezya Huvisa akizungumza na waandishi wa habari ofisin kwake jijini dar es salaam leo kuhusu tamko la serikali la upigaji marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchi.(Picha na Ofisi ya Makamu ya wa Rais.)

Na Ofisi ya Makamu wa Rais

Serikali imepiga marufuku ungizaji, utengenezaji, uuzaji, na utumiaji wa mifuko ya plastiki. hayo yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais(mazingira) Dk Terezya Huvisa alipokuwa akizungumza na waandishi ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.

Dkt. Hufisa ameeleza kuwa Serikali imehamua kuchukua hatua hii ili kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la kusambaa na kutapakaa kwa taka za mifuko ya plastiki ambayo baada ya matumizi yake huishia kwenye uchafuzi wa mazingira .

Alisisitiza kuwa, Zuio hili linahusu mifuko yote ya Plastiki ya kubebea bidhaa toka madukani, sokoni na majumbani isipokuwa mifuko yenye unene wa maikroni mia moja inayooza (bio-digradable) na vifungashio vya bidhaa mbali mbali kama vile vifaa vya mahospitalini.

“Marufuku hii inapaswa kuzingatiwa na wenye viwanda, wenye maduka na wananchi kwa ujumla ili kutokomeza kuenea kwa taka zinazotokana na mifuko ya plastiki kwenye mazingira.” Alisema.

Dkt Hufisa aliendela kusema kuwa, Jitihada zinatakiwa zifanywe ili kuhakikisha kuwa marufuku hii inazingatiwa, na misako ya watu wanaofanya biashara ya mifuko hii ifanyike katika maeneo yote ndani ya nchi yetu, na watakaokiuka wachukuliwe hatua, ikiwa ni pamoja na kufanikishwa katika vyombo vya sheria .

Imeelezwa kuwa madhara yanayosababishwa na mifuko ya plastiki ni pamoja na uharibifu wa udongo unaotokana na kuunguzwa kwa plastiki hizi na hivyo kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama ,kutooza kiurahisi wa njia za kiasili (non-biodegradable) kuzagaa katika mito, maziwa, bahari na nchi kavu hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai wanaoishi katika mazingira.
Read More >>

Wednesday, July 31, 2013

Kama huyu anaweza kufanya hivi, hakuna atakaeshindwa

image

Kwa nchi kama Tanzania sio ajabu kabisa kushuhudia mtu akitupa takataka kwenye mazingira ambayo hayaruhusu kabisa mfano yuko kwenye gari inatembea anatupa chupa ya maji au uchafu mwingine wowote.. kuna uwezekano hii picha ikabadilisha tabia ya mtu wa aina hii akiiona.
Huyu ni kunguru ambaye alionekana akiokota kopo la soda likiwa limezagaa na akaamua kuliokota na kuliweka mahali sahihi, kwenye ndoo maalum ya takataka… tufate mfano wake, kuna uwezekano kabisa ukiwa na uchafu ukaubeba mpaka sehemu maalum ya kutupa taka.
Read More >>

Saturday, July 27, 2013

MAFUTA YA UBUYU HATAMBULIWI NA SERIKALI KUWA TIBA

Picture: 
Baobab oil, mafuta ya ubuyu WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema bado haitambui mbegu za ubuyu kuwa zinatoa mafuta ambayo ni tiba. Aidha imesema inatambua kuwa tiba kutokana na mti huo ni majani, magome na unga wa ubuyu.

Wizara pia imeitaka jamii kuwa macho na waganga wa tiba za asili na tiba mbadala ambao hawajasajiliwa kwa kuwa kama zilivyo dawa nyingine, tiba ya asili ina madhara yanayoweza kuleta matatizo makubwa katika maisha ya mtu kama haijapimwa na kuthibitishwa.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Paulo Mhame aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika semina ya siku moja kuhusu masuala ya tiba asili na tiba mbadala nchini.

Akizungumzia ubuyu, baada ya kuulizwa swali kama ni sahihi mafuta ya ubuyu kutumiwa kama tiba Dk Mhame alisema Serikali haitambui mafuta ya ubuyu kama tiba.

Alisema mti wa ubuyu unatumika kama tiba kwa baadhi ya mazao yake kuchanganywa na vitu vingine na kutoa dawa ikiwemo majani, magome yake na unga wa ubuyu wenyewe, lakini mpaka sasa hakuna taarifa ya kitaalamu kuhusu mafuta ya ubuyu kuwa dawa.

Dk Mhame alisema nchi za Magharibi zimekuwa zikinunua mafuta ya ubuyu kutoka Afrika kwa ajili ya kutengeneza vipodozi: “Nchi za Ulaya zimekuwa zikinunua mafuta ya ubuyu kutengeneza vipodozi, mtu mwenye miaka 90 anataka kuonekana ana miaka 60,” alifafanua Dk Mhame.

--- Gloria Tesha/HabariLeo
Read More >>

Thursday, July 18, 2013

PICHA: MADHARA YA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA

 
Read More >>

Wednesday, July 17, 2013

PICHA: WAGONJWA MUHIMBILI WALAZWA NJE ILI KUUA WADUDU

 Wagonjwa wakiwa nje huku wengine waipata tiba baada ya kutolewa wodini kupisha upuliziaji wa dawa ya kuua wadudu katika majengo ya Kibasila na Mwaisela Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam. PICHA NA MDAU KHAMIS MUSSA






Read More >>

Saturday, July 13, 2013

MOI yajibu madai ya bodaboda kukatwa mguu


Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MOI), inayodaiwa kuchangia kuongeza ‘ walemavu’ kwa kuwakata viungo majeruhi wa ajali za boda boda, imesema ipo tayari kuthibitisha kuwa waliokatwa viungo si madereva wa pikipiki kama inavyodaiwa.  “Anayetaka kufahamu ukweli tuwasiliane.Takwimu za waliokatwa  miguu na viungo zipo hatuna cha kuficha  tena si madereva wa pikipiki  kama inavyodaiwa,” Ofisa Uhusiano wa  MOI, Almasi Jumaa, alisema.


Wanaotoa tuhuma hizo wanadai wodi ya kuchangia huduma, waganga wanawakata  miguu majeruhi wengi  wa ajali  za bodaboda na hulazwa kwenye wodi maalumu zinazojulikanazo kiutani kama  ‘boda boda na Sanlg’ .
Akijibu madai hayo Jumaa aliongeza:“uamuzi wa kumkata majeruhi kiungo haufanywi kinyemela ni makubaliano ya jopo la madaktari,  hukatwa kiungo  baada ya  daktari wa mgonjwa kupendekeza kwa wakuu wake  ambao huwasiliana na mabingwa wanaomchunguza mgonjwa na kuridhika kuwa  ili kuokoa maisha yake wanalazimika kuondoa kiungo.”
Alisema majeruhi wanaopokelewa MOI wanatibiwa  na kuhudumiwa bila kubaguliwa  na kwamba hakuna wodi ya boda boda wala Sanlg na anayetaka uhakika afike MOI kuthibitisha.
Aliongeza kuwa ukataji viungo huzingatia viwango vinavyokubaliwa kimataifa na kwamba unafanyika pale ambapo mgonjwa ameumia na hawezi kutibika.
Katika mahojiano na baadhi ya majeruhi na jamaa zao hospitalini hapo walibainisha kuwa hawaridhishwi na moyo wa madaktari na wauguzi katika kuhudumia wagonjwa.
Majeruhi wa boda boda walisema madaktari wanawapuuza, huchelewa kuwatibu hali inayowasababishia maumivu makali licha ya kwamba wapo hospitalini.
Walisema kutotibiwa kwa haraka husababisha viungo kuharibika,  kukatwa
na wengine kupoteza maisha na kudai kuwa katika wodi  ya wagonjwa wanaochangia huduma za afya, majeruhi hulundikana kupindukia.
Walisema baadhi huambukizwa hata maradhi  ya wodini  pia kuna harufu mbaya inayotokana na ama vidonda vyenye usaha sivyosafishwa au uchafu wa shuka zilizochafuliwa na damu na pia majeruhi  kutooga kutokana na kuumia viungo.
Walidai madaktari huwakimbia wagonjwa wakitoa mfano kuwa ukifika hospitalini hapo unapewa daktari atakayekuelekeza vipimo na dawa.
Hata hivyo  baadaye tabibu huyo hutoweka na mgonjwa  kupigwa dana dana na kulazimika kumtafuta mwingine ambaye anakerwa na kuhoji sababu za kukimbiwa na daktari wake hali inayomfanya mgonjwa kutapatapa kusaka huduma.
Walisema jamaa za wagonjwa huzunguka kila mahali kuwatafuta madaktari ambao nao hawaonekani.
Walidai MOI haina dawa na pia hakuna gozi wala dawa za maji za kusafishia vidonda.
Baadhi walidai hakuna umakini wa kumfuatilia mgonjwa ambaye anaweza kuvalishwa mhogo (pop) mara kadhaa na mguu wake usiunge.
Pia walidai iliwahi kutokea  baadhi ya wataalamu wa dawa ya usingizi (nusu kaputi) walimwekea mgonjwa dawa kidogo na kusababisha kuzinduka kabla ya upasuaji kukamilika.
“Walilazimika kumuongezea mgonjwa  nusu kaputi iliyomzidia na kusababisha kifo ,” alidai mgonjwa  mmojawapo.
UFAFANUZI 
Akijibu malalamiko hayo  Jumaa alisema  wodi ya wagonjwa wa kuchangia huduma ina vitanda 33 lakini idadi ya majeruhi wanaolazwa inafikia zaidi ya 60 hali inayosababisha  mlundikano na harufu wodini.
Alitoa takwimu za wagonjwa zilizoonyesha kuwa kati ya 1996-1997 waliolazwa walikuwa  5,000 wakati wagonjwa wa nje walikuwa 6,700 na kwa  mwaka 2011 na 2012 wagonjwa waliolazwa walikuwa 7,070 wakati wa nje walikuwa  62,000.
Alisema hospitali hupokea  majeruhi angalau 10 kila siku na kwamba kila ajali kubwa majeruhi hufikishwa MOI hali inayosababisha msongamano na foleni  hata kwenye upasuaji.
Alisema hakuna uhaba wa madaktari wa mifupa na kuhudumia wagonjwa wa ajali kama inavyodaiwa na kwamba taasisi hiyo inawasaidia majeruhi  kwa kuwapa tiba,chakula na hata kuwafikisha kwao wakipona.
habari NA GAUDENSIA MNGUMI
CHANZO: NIPASHE
Read More >>

Wednesday, July 10, 2013

WANAOSUMBULIWA NA VIDONDA VYA TUMBO DAWA HII HAPA.


 
MTABIBU WA DAWA ZA ASILI WA MAASAI NATURAL MEDICINE, KIM NIUYAI.
DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO (LETHI) DOZI YAKE NI SIKU MBILI TU NA UTAPONA KABISA.
PIA TUNATIBU MAGONJWA MENGINE YAKIWEMO MAGONJWA YA KISUKARI, KAN
SA (CANCER) YA AINA YEYOTE, PRESHA (PRESSURE), PUMU, GOUT,CHOLESTEROL, MALARIA, TYPHOID NA VIDONDA VYOTE.
MAGONJWA YA MIGUU, INI, FIGO, MOYO, UTI, FANGASI, MATATIZO YA MBEGU ZA KIUME (OLIGOSPERMIA), MBEGU ZA KIKE (HORMONES), NA MAGONJWA MENGINE MENGI.

KWA USHAURI NA TIBA:  
TUNAPATIKANA KATIKA STENDI YA KABWE JENGO LA OTTU CHUMBA NO 54 MBEYA MJINI. 
UTAONA BANGO AMBALO LIMEANDIKWA "MAASAI NATURAL MEDICINE", PIA TUNAWEZA KUMTUMIA YEYOTE ANAYEHITAJI DAWA POPOTE ALIPO NCHINI NA HATA NJE.
KWA MAWASILIANO WASILIANA NASI KWA NAMBA ZA SIMU:  
0713 690 999, 0767 225 566 AU 0765 018 998, 0786 018 998
Read More >>

Monday, July 8, 2013

ANGALIZO:MAFUTA YA UBUYU YANA TINDIKALI INAYOSABABISHA SARATANI

Baada ya kuonya wananchi wanaotumia dawa za tiba mbadala ambazo hazijathibitishwa, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania(TFDA), sasa inawataka wananchi kuacha kutumia mafuta ya ubuyu kwa kunywa kama dawa.
Akizungumza juzi katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza, alisema Mamlaka hiyo ilipima na kubaini mafuta hayo yana tindikali ya mafuta.
Alifafanua katika maonesho hayo maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, kwamba mafuta hayo hayafai kuliwa na binadamu na anayekunywa kwa wingi, yuko hatarini kupata saratani za aina tofauti tofauti. 
"Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wajasiriamali wanaouza mafuta ya ubuyu kama dawa, kwa kuwaelekeza wananchi kunywa. Napenda kuwataarifu kuwa mafuta hayo ni hatari kwani yana tindikali ya mafuta," alisema.


Mwandishi alipata sampuli ya vielelezo vya matumizi yake na manufaa yake mwilini, kama inayotangazwa na wajasiriamali katika maeneo mbalimbali na hata katika mitandao. 


  
"Ni mafuta yatokanayo na mbegu za ubuyu {au kokwa}. Hukamuliwa kiini chake na kutoa mafuta. Yana ubora kuliko mafuta mengine ya kupikia, yana Vitamin A, B, C, D na F. Pia yanatibu magonjwa mbalimbali," kielelezo kimoja kilinadi ubora wake katika mitandao ya jamii.



Mafuta hayo yamedaiwa kutengeneza seli zote ndani ya mwili, kuzuia ngozi isiharibike wala kupata makunyanzi, kuondoa mafuta  ndani ya mishipa ya damu na yanapunguza uzito uliozidi.


Pia inadaiwa yanarutubisha ini na figo, yanaleta hamu ya kula, yanaimarisha mifupa, kucha na nywele, yanaongeza kinga ya mwili (CD4), yanaondoa sumu na yanatengeneza sukari iwe katika kiwango kinachotakiwa.

Maelezo hayo yameendelea kusifu kwamba yanasaidia kuona vizuri na kujenga kumbukumbu, yanapunguza vitambi na matumbo makubwa, yana virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini.




Katika ngozi yametajwa kuondoa madoa, chunusi, fangasi, upele, mba na muwasho, yanafaa kwa walemavu wa ngozi (albino). Pia huondoa hamu ya kutumia dawa za kulevya na kuponyesha vidonda vya tumbo.


"Endelea kutumia mafuta bora ya ubuyu, ni bidhaa asilia ya kitanzania. Ni mafuta yasiyochanganywa na kitu chochote, ni mafuta asilia,"  yamesifiwa katika maelezo hayo.


Mtumiaji ameelezwa kama ana ugonjwa wa kisukari, atumie kijiko cha chakula kimoja tu. Anatakiwa kutumia dozi hiyo ya kwanza nusu saa kabla ya kula chochote kwa muda wa siku 15.

Dozi ya pili na ya tatu kwa wagonjwa hao, inatakiwa kufuata baada ya siku 15 kisha mgonjwa apumzike wiki moja, huku akiendelea kupima kila wiki. Kipimo hapo ni cha hospitali.



Kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo, figo na ini, wameelekezwa na wajasiriamali hao kunywa kijiko cha chakula kimoja asubuhi kabla ya kula chochote, na usiku kijiko cha chakula kimoja kabla hajala chochote kwa muda wa siku 15 kwa dozi ya kwanza.


Baada ya hapo, mgonjwa anapumzika wiki moja kisha siku 15 zinazofuata dozi ya pili, mapumziko wiki moja halafu siku 15 nyingine dozi ya tatu. 


Maelezo ya dozi hiyo ya kutibu ugonjwa wa vidonda vya tumbo, yanaendelea kumtaka mgonjwa baada ya dozi ya tatu, aanze kunywa kila wiki mara moja kijiko cha chakula kimoja asubuhi, tena nusu saa kabla hajala chochote kwa muda wa wiki nne.


Dozi inaendelea ambapo mgonjwa atatakiwa kunywa kijiko kimoja cha chakula kila mwezi mara moja asubuhi, kabla hajala chochote kwa muda wa wiki nne, kisha kunywa kila mwezi mara moja, asubihi kabla hajala chochote kwa muda wa miezi sita mfululizo.


Kwa utoaji wa sumu, mgonjwa ametakiwa kunywa kijiko cha chakula kimoja asubuhi kila siku kwa muda wa siku 14, kisha kunywa kila mwezi mara moja kwa muda wa miezi sita mfululizo.

Kwa kuongeza CD4 mwilini, ametakiwa kupata kijiko cha chakula kimoja asubuhi nusu saa kabla ya kula chochote, na usiku kijiko cha chakula kimoja nusu saa kabla ya kula chakula cha usiku kwa muda wa miezi mitatu. 




"Mgonjwa aanze kunywa baada ya kipimo cha mwisho (cha CD4) alichopima. Mafuta yanapatikana kuanzia ujazo wa lita moja na zaidi," imesifiwa dawa hiyo.


TFDA imeonya kuibuka kwa tabia ya wananchi kutaka matibabu ya haraka, kama ilivyo kwa baadhi ya watu kutaka utajiri wa haraka, na imehadharisha ni vema kabla ya kutumia dawa zinazoibuka kila siku, waulize kama zina ubora kwa afya zao.


"Nawasihi wananchi kuacha kukimbilia dawa ngeni mara tu baada ya kutangazwa kama haya Mafuta ya Ubuyu, yamekuwa yakielezwa ni dawa na wajasiriamali tu, na wengi wamekuwa wakitumia bila kusikiliza mamlaka husika zinasemaje," alisisitiza.


Semwanza alisema Mamlaka hiyo iko katika mkakati wa kuanza kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya mafuta hayo, ambayo wengi wanayaamini na kuyanywa kama dawa.


Kwa mujibu wa Semwanza, baada ya kupima mafuta hayo na kubaini hatari hiyo, waligundua pia inawezekana tindikali hiyo kutenganishwa na mafuta hayo, lakini imebainika utaalamu na teknolojia hiyo haipo nchini.


Hata hivyo, alisema Mamlaka hiyo haijabaini madhara ya matumizi mengine ya mafuta hayo kama kipodozi.


Kutokana na mvuto huo wa kibiashara, na shauku ya kupona haraka ya wananchi, Semwanza alisema TFDA imekuwa ikifanya msako wa dawa mbalimbali zinaouzwa na wajasiriamali katika maonesho hayo.

Alisema kuwa kuna baadhi ya waandaaji wanaowaalika wajasiriamali bila kufuata kanuni na sheria za kuingiza dawa hizo katika maonesho.


Kwa mujibu wa Semwanza, wanakagua dawa na kama wakikuta hazijathibitishwa na TFDA na mamlaka nyingine, wanamuamuru mjasiriamali kuacha kuzitangaza mpaka apate kibali na kuwaasa wanaowaleta wajasiriamali katika maonesho hayo ya kimataifa kuhakikisha wanafuata vigezo.

Wiki iliyopita TFDA, ilionya wananchi dhidi ya matumizi ya dawa za tiba mbadala, zikiwamo zinazokuza maumbile, ambazo bado hazijasajiliwa na Mamlaka hiyo baada ya kuchunguza usalama, ubora na ufanisi wa dawa hizo.



Mamlaka hiyo  ilieleza kuwa, ilitoa nafasi ya watoa tiba mbadala kwenda kusajili dawa zao, lakini mwitiko umekuwa hafifu. 

  
TDFA yenye dhamana ya kusimamia ubora na usalama wa bidhaa za vyakula na dawa, ikiwa ni pamoja na dawa za mitishamba, vipodozi na vifaa tiba vinavyouzwa katika soko la Tanzania, imeeleza kuwa watoa huduma wa tiba mbadala, wengi hawako tayari kubainisha aina ya mchanganyiko wa dawa hizo jambo ambalo ni hatari kwa walaji.

Read More >>
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...