Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume wengi waliokuwa wakimsaidia wakati
mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka
kimapenzi.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini
ya Zamaradi Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa
karibu naye wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka
kimapenzi, jambo ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.
Bishosti huyo alisema kuwa tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa
sapoti kipindi hicho, bado wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya
nchi ambao wanatuma maombi kwake lakini anawaona wote ni matapeli na
wanamtamani tu hivyo hayupo tayari kuingia kwenye uhusiano wa aina hiyo.
“Kweli ninaumia sana kwa sababu ninakaa na kujiuliza hawa wanaume
walikuwa wanasubiri mume wangu afariki dunia ndiyo wanitongoze?
“Kusema kweli inanishangaza, hata watu ambao sikuwadhania kabisa eti nao
wananitaka, watu wajue kwa sasa sipo tayari kuwa na mwanaume.
“Sitaki kukurupuka kwa sababu naweza nikaingia kwenye shimo la taka
kwani jamii itanikimbia kutokana na kunuka, natamani kumpata mwanaume
anayefanana na mume wangu kitabia.
“Uvumilivu wangu na uzuri ulitokana na kutunzwa siyo aje mtu anayetaka
nikavumilie shida, hilo sitaki litokee, namuomba Mungu sana,” alisema
Wastara.