Wodi ya wajawazito hospitalini hapo. |
Wanawake
masikini wamekuwa wakinyonywa katika wakati wao usio salama na hospitali
moja ambayo huwatoza Dola za Marekani 5 kila wanapopiga kelele wakati
wa kujifungua.
Uvumbuzi
huo wa kushitusha ulifanywa na kundi la Wamarekani linalofanya kampeni
dhidi ya rushwa, iliposambaza ripoti yake ya kila mwaka Global
Corruption Barometer.
Katika
hospitali hiyo nchini Zimbabwe, moja ya nchi masikini kabisa duniani,
faini hiyo ilisemekana kutozwa kwa 'kupiga king'ora kimakosa', kwa
mujibu wa Transparency International.
Wanawake
ambao hawakuwa na uwezo wa kulipa faini hiyo walidaiwa kufungiwa
hospitalini hapo hadi familia zao zitakapokuja kulipa. Riba pia
huongezwa kwenye faini hizo, kwa mujibu wa ripoti hizo.
Akinamama
wengi tayari wamekuwa wanakwepa kujifungulia hospitalini katika taifa
hilo la Afrika sababu ya gharama hiyo ya Dola za Marekani 50, ambayo ni
takribani theluthi moja ya wastani wa kipato cha Dola za Marekani 150.
Na Ziro
Katika
nchi ambako karibu asilimia 95 ya idadi ya watu wote hawana ajira baada
ya miaka kadhaa ya mtikisiko wa uchumi na rushwa chini ya Rais Robert
Mugabe, na mmoja kati ya wanawake wanane hufa wakati wa kujifungua kila
siku, faini hizo zinapora mshahara wa mwanamke wa mwaka.
Utafiti wa Wazimbabwe umegundua asilimia 65 inaamini huduma za matibabu nchini humo zimetawaliwa na rushwa.
Pale
Transparency International ilipowasiliana na Naibu Waziri Mkuu wa
Zimbabwe, aliamuru uchunguzi ufanyike na tangu hapo hakuna ripoti zozote
za faini zilizopatikana.
Hatahivyo, gharama ya Dola za Marekani 50 wakati wa kujifungua imeendelea kuwapo.
Kundi
hilo la kampeni sasa limeandaa warsha kashaa nchini Zimbabwe kuinua
uelewa kuhusu rushwa na kuonesha wananchi jinsi maofisa rekodi
wanavyotaka hongo hivyo kuweza kutoa ushahidi mahakamani.
Faini
wakati wa kujifungua zilianikwa wakati kundi hilo la kampeni lilipotoa
ripoti ikionesha kwamba karibu robo ya watu wote duniani imetoa hongo
katika mwaka uliopita.
Ugunduzi
huo, uliolenga kwenye utafiti kwa watu 100,000 katika zaidi ya nchi 100,
uligundua kwamba polisi na mifumo ya mahakama ilikuwa ikiongoza kwa
rushwa, kwa mujibu wa ripoti.
Karibu theluthi ya watu ambao walishiriki kwenye utafiti walisema walitoa hongo kwa polisi.
Nchi ambayo kinara wa rushwa ilikuwa Sierra Leone, ambako asilimia 84 ya watu waliohojiwa waliripoti kutoa hongo.
Nafasi ya mwisho kwa rushwa ilishikwa kwa pamoja na nchi za Australia, Denmark, Finland na Japan.
Katika nchini ya Marekani, asilimia 7 ya wote waliohojiwa walidai kuwahonga polisi, iliripotiwa.