Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Hofu
kubwa ya kutokea tena kwa vurugu katika uchaguzi mdogo wa madiwani
kwenye kata nne imeugubika mji wa Arusha na vitongoji vyake.
Hofu
hiyo inatokana na ugumu wa uchaguzi huo pamoja na mlipuko wa bomu
uliotokea mwezi uliopita mkoani humo katika mkutano wa kufunga kampeni
za udiwani kwa CHADEMA na kuua watu wanne na kujeruhi wengine 70.
Tanzania
Daima imedokezwa kuwa uchaguzi huo utakuwa na mvutano mkubwa kwa vyama
vya CHADEMA na CCM ambavyo idadi ya madiwani wao inakaribiana sana, na
ndio utakaoamua nani ataiongoza Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, CCM ilikuwa na madiwani 10 wa kata, viti
maalumu watatu na wabunge watatu na jumla yao kuwa 16.
CHADEMA
nao walipata madiwani wanane wa kata, viti maalumu watatu na wabunge
watatu, jumla 14, huku TLP wakiwa na madiwani wawili.
Baada ya
matokeo hayo, ulifanyika uchaguzi wa meya na naibu wake, ambao
ulitawaliwa na vurugu kubwa, huku CHADEMA wakikataa kumtambua Meya
Gaudence Lyimo (CCM).
CHADEMA
waliamua kufanya maandamano ya kupinga mchakato uliomuwezesha meya huyo
kuingia madarakani na kuzuka vurugu zilizosababisha polisi kuwaua kwa
risasi watu watatu.
Tangu
wakati huo hadi sasa, mji wa Arusha na viunga vyake haujapata utulivu
wa kisiasa, huku CCM ikidaiwa kuendesha harakati za kuidhoofisha CHADEMA
na Mbunge wake, Godbless Lema, anayeonekana kuwa mwiba mkali.
Hata
hivyo, CCM ilipata ahueni mwaka 2011 pale CHADEMA ilipoamua kuwafukuza
uanachama madiwani wake watano kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.
Madiwani
wanne walikuwa wa kata na mmoja wa viti maalumu. Madiwani hao ni Diwani
wa Kimandolu, Estomih Mallah, Diwani wa Elirai, John Bayo, Diwani wa
Themi, Ruben Ngowi, Diwani wa Kaloleni, Charles Mpanda na Diwani wa Viti
Maalumu, Rehema Mohamed.
CCM
nayo ilipata pigo mwaka jana baada ya diwani wake wa Daraja Mbili
kufariki dunia, huku diwani wa Sombetini, Alphone Mawazo, akiamua
kujiunga na CHADEMA, na hadi sasa kata yake haijatangazwa kuwa wazi kwa
sababu ambazo hazijawekwa wazi.
Kinachogembewa
CHADEMA
na CCM ugomvi wao mkubwa kwa Jiji la Arusha ni kuongoza halmashauri
hiyo na kutoa meya, hivyo uchaguzi wa keshokutwa ndio utaamua majaliwa
ya nafasi ya meya aliyepo hivi sasa anayetoka chama tawala.
Uchaguzi
huo unatarajiwa kuwa mgumu zaidi kwa pande zote mbili kutokana na
kupungua kwa idadi ya madiwani, tofauti na ilivyokuwa mwaka 2010.
Safari hii CCM ina madiwani wanane wa kata, madiwani wa Viti Maalumu watatu na wabunge watatu ambapo jumla yao ni 14.
CHADEMA wenyewe wana madiwani watano wa kata, viti maalumu watatu na wabunge watatu, ambapo jumla yao ni 11.
Kama
CHADEMA itafanikiwa kurejesha kata zake nne, itakuwa na madiwani wa
kata tisa, wabunge watatu na madiwani wa viti maalumu watatu, hivyo
kufanya idadi yao kuwa 15, hivyo kuwazidi CCM kwa diwani mmoja.
Idadi
hiyo itawafanya wawe na uwezo wa kuongoza halmashauri hiyo na kutoa
meya wa jiji hilo, kwani wakiingia kwenye baraza la madiwani wanaweza
kumng’oa wa CCM na kumchagua wa kutoka chama chao.
CCM
wanaweza kulingana na CHADEMA kama watafanikiwa kumshawishi Diwani wa
TLP, Michael Kivuyo, kuwaunga mkono kwenye kura za umeya, hivyo pande
hizo kila moja kuwa na madiwani 15.
Kama
hali itakuwa hivyo, pande hizo mbili zitalazimika kukaa kwenye meza ya
mazungumzo kukubaliana utaratibu wa kuongoza halmashauri ya jiji kwa
kupokezana kwa kipindi fulani.
Wachambuzi
wa masuala ya siasa wamelidokeza Tanzania Daima kuwa uchaguzi wa kesho
kutwa utakuwa mgumu zaidi kuliko ilivyowahi kutokea huko nyuma.
Tayari
kuna taarifa kuwa idadi kubwa ya viongozi wa CCM wamepiga kambi mkoani
humo kuhakikisha wanapata walau kata moja au mbili ili kuendelea
kuiongoza halmashauri ya jiji hilo ambalo ni kivutio kikubwa cha utalii.
Ugumu wa uchaguzi huo
Ugumu
wa uchaguzi huo pia unachangiwa na mlipuko wa bomu uliotokea mwezi
uliopita kwenye mkutano wa kufunga kampeni wa CHADEMA, ambapo watu wanne
walifariki dunia na 70 kujeruhiwa.
Baadhi
ya watu waliozungumza na Tanzania Daima walionesha wasiwasi wao juu ya
usalama siku ya uchaguzi huku wengine wakieleza kuwa wanahofia
kujitokeza siku ya kupiga kura.
Simon John, mkazi wa Kata ya Themi alisema bado ana hofu ya kujirudia kwa matukio ya kupigwa mabomu kama yalivyojitokeza awali.
Joyce
Tumaini, mkazi wa Kimandolu alisema mlipuko wa bomu uliotokea mwezi
uliopita unaweza ukasababisha watu wachache kujitokeza kupiga kura.
Usalama safi
Mkurugezi
wa Jiji la Arusha, Sipora Liana, amewataka wakazi wa jiji hilo
kujitokeza kwa wingi kuhitimisha uchaguzi mdogo wa kata nne zilizosalia
baada ya uchaguzi huo kuahirishwa awali kutokana na mlipuko wa bomu
uliotokea Juni 16 na kuua watu wanne na wengine 70 kujeruhiwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini hapa, Liana alisema hali ya usalama
imeimarishwa na hakuna hofu ya kutokea milipuko katika uchaguzi huo
aliosema utaanza saa 1 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Alitaja
kata zitakazochagua madiwani wao kuwa ni Kaloleni, Themi, Kimandolu na
Elerai, huku akiainisha kuwa vituo katika kata zote ni 136 na kila kituo
kitakuwa na msimamizi mmoja.
Aliongeza
kuwa wapiga kura waliojiandikisha ni 60,123 na kwamba wamekubaliana na
viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo kuwataka wafuasi wao kuondsoka
katika maeneo ya kupigia kura baada ya zoezi hilo kukamilika kwa kila
mmoja.