Lil Twist, mshkaji wa karibu sana wa Msanii Justin Bieber ambaye pia ndiye anahisiwa kuwa bad influence kwake, ameingia tena kwenye kisa kingine baada ya kukamatwa na polisi akiwa anaendesha gari ya Bieber [Fisker Karma] katika hali isiyokuwa ya kawaida - dalili zote zikiwa zinaonyesha kuwa kuna kitu ametumia kidogo ambacho kilikuwa 'kimetwist' akili yake >>>>> mos definitely 'tungi'. |
Twist amekamatwa mida mibovu, saa 9 na nusu usiku, na kosa la kwanza lililopelekea yeye kusimamishwa ni kuendesha gari hii kwa mwendo kasi akiwa anaelekea nyumbani kwa Bieber na msanii huyu alichukuliwa hadi kituo cha polisi cha karibu na hadi sasa bado haijawekwa wazi kuwa ni hatua gani amechukuliwa.