Stars
ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009
ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa
Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao
1-1.
Wenyeji ndiyo walioanza kufunga bao
dakika ya saba katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee
kutoka Madagascar. Frank Kalanda alifunga bao hilo akimalizia mpira
uliopigwa ndani ya eneo la hatari la Tanzania.
Bao hilo halikuonekana kuichangaza Taifa
Stars, kwani ilitulia na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18 mfungaji
akiwa Amri Kiemba kutokana na pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye kona ya
eneo la mita 18.
Dakika
ya 32 nusura Taifa Stars ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Mrisho
Ngasa ambao tayari ulikuwa umempira kipa HAmza Muwonge uligonga mwamba
kabla ya kuokolewa na mabeki wa Uganda Cranes.
Mabao
mengine ya Uganda Cranes yalifungwa dakika ya 48 kupitia kwa Brian
Majwega na lingine dakika ya 63 mfungaji akiwa tenda Kalanda kutokana na
makosa ya Salum Abubakar kupokonywa mpira wakati akiwa katika nafasi
nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.
Kocha
Kim Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 43 kwa kumuingiza Simon Msuva
badala ya Frank Domayo aliyeumia, na dakika ya 78 akawaingiza kwa mpigo
Haruni Chanongo na Vincent Barnabas badala ya David Luhende na John
Bocco. Hata hivyo mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo.
Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Juma
Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende/Vincent Barnabas, Aggrey Morris,
Kelvin Yondani, Athuman Idd, Frank Domayo/Simon Msuva, Salum Abubakar,
John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itarejea nyumbani kesho
(Julai 28 mwaka huu) saa 4 usiku kwa ndege ya PrecisionAir.