Mtanzania pekee anayeiwakilisha Tanzania
kwenye ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani maarufu kama NBA, Hasheem
Thabeet. Hivi karibuni alijunga na majaji wa Bongo Star Search kwa
lengo la kuwapa moyo vijana ambao wanajaribu kuonyesha vipaji vyao
kwenye shindano hili. Hasheem Thabeet ni moja ya vijana ambao
wamefanikiwa kutumia vema vipaji vyao na kuwa mfano mzuri kwa vijana
wengine kufanya juhudi kwenye talent zao.
Jaji mkuu wa BSS Rita Paulsen aliandika kupitia ukurasa wake wa facebook kwamba, “Rafiki
yangu Hasheem Thabeet alikuja kuwapa moyo na kuonyesha support yake kwa
vijana wanaofanya usaili. Namshukuru sana kwa mchango wake”.