Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, July 15, 2013

SOMA ALICHOKIANDIKA RAY KUHUSU MAREHEMU KANUMBA

Steven Kanumba, Vincent Kigosi



Maswahiba wawili wakitoka safari marehemu Kanumba na Ray


MWIGIZAJI, mtayarishaji na muongozaji mahiri wa filamu Swahiliwood Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’ hivi karibuni aliangusha bonge la sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuwakaribishwa rafiki zake na wadau wa filamu katika moja ya Hotel, siku hiyo pia aliweza kumkumbuka swahiba yake marehemu Kanumba na kuhisi uenda angekuwepo siku hiyo.

.
“Ni siku ambayo nimesheherekea siku yangu ya kuzaliwa na ndugu zangu wa karibu na wasanii wenzangu, ni siku ambayo nimekumbuka mambo mengi sana katika maisha yangu, mara nyingi swahiba wangu marehemu Kanumba siku kama ya leo ningekuwa naye katika sherehe kama hii, lakin ndio mambo ya Mungu huwezi kulaumu kilichobaki ni kumuombea Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani Amen,” alisema The Greatest.
Katika sherehe hiyo iliyopambwa na vinywaji na malaji kibao ilijumuisha wasanii nguli katika tasnia ya filamu kama Bonge la bwana, JB, Maya, Odama, Chikoka na wasanii wengine kibao huku kukiwa na michezo kadha wa kadhaa ni jambo jema kwa marafiki kukumbuka katika matukio kama hayo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...