Jina
lake anaitwa Danny David ni Mwanamitindo wa kume toka Tanzania na
mwanamitindo pekee toka Tanzania alipata nafasi ya kufanya kazi ya
kutangaza nguo na viatu vya kampuni kubwa ya Adidas tawi la Afrika ya
kusini.
Alianza
kuonekana kwenye fashion mwaka 2012 kwenye maonesho ya Swahili Fashion
Week chini ya mwanamitindo maarufu nchini Mustapha Hasanali, ameshiriki
kuonesha mavazi kwenye Harusi fashion week iliyofanyika chini ya mbunifu
wa mavazi Ally Rehmutula na pia alishawahi kushiriki na kushinda kwenye
mashindano ya wanamitindo ya Maridadi model search yaliyofanyika hapa
Tanzania.
Danny
ni mwanasheria kitaaluma na ana degree ya sharia toka chuo cha Tumaini
Iringa Katika interview tuliyofanya naye hivi karibuni Danny amesema
pamoja na kuwa mwanamitindo anamipango ya kuwa muigizaji kwani ni kitu
alichokuwa anapenda kukifanya tangu utotoni.