Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, July 15, 2013

HATIMAYE PREZZO AMUOMBA MSAMAHA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUMDISS.STORI NZIMA HII HAPA

                                  page
 

Diamond Platnumz amesema Rapcellency Prezzo alimpigia simu hivi karibuni kumuomba msamaha kufuatia tweet za kumdiss alizoziandika wiki iliyopita, lakini hitmaker huyo wa Kesho amesema kama Prez ana nia ya kumuomba msamaha basi afanye...... hivyo hadharani kwenye mtandao wa Twitter.
 
Diamond alikuwa akihojiwa mchana wa leo kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen ya nchini Kenya kinachoendeshwa na mtangazaji William Tuva. Msanii huyo anayeongoza kwa kulipwa zaidi kwenye show nchini, amesema alishangazwa na kitendo hicho cha Prezzo kumdis kutokana na majigambo aliyoyatoa kabla ya show yao kwenye Tamasha la Matumaini mwanzoni mwa mwezi huu. Amesema haoni sababu ya Prezzo kuyachukulia vibaya majigambo hayo kwakuwa hayakuhusiana na maisha ya kawaida bali ni ya kawaida kwa show za kupambanishwa na kutolea mfano jinsia wacheza mieleka wnavyotambiana kwenye mechi zao na kwamba kwenye maisha ya nje huwa hawana ugomvi. “Sikujisikia vizuri kabisa, vitu vingi vimezungumzwa, kwanini anitukane, mimi sijazoea mambo hayo,” amesema Diamond. “Tuache mambo ya zamani ya kutengeneza attention kupitia ugomvi, tutengeneze ngoma kali, haina haja ya kugombana.” Diamond ametoa ushauri kwa wasanii wote Afrika Mashariki kuwa wanatakiwa kuungana ili kuupeleka juu muziki wake ili kwenda sawa na wanamuziki wa Afrika Magharibi.
“Sikupenda kama binadamu wa kawaida, sikujisikia vizuri, East Africa hatuna muda wa kugombana.” Aliongeza kuwa majigambo ya wasanii kuhusu kuzidiana fedha hayana maana yoyote.”Hakuna mwanamuziki mwenye hela East Africa, tufanye kazi nzuri kuleta sifa kwenye nchi zetu.” Hata hivyo amesema licha ya kuumizwa na kitendo hicho cha Prezzo, hana tatizo naye. Katika hatua nyingine, Diamond amesema yuko mbioni kufanya ngoma na Jose Chameleone wa Uganda
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...