Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Saturday, July 13, 2013

RED BRIGADE YA CHADEMA NI KUNDI LA KIGAIDI : MWIGULU NCHEMBA

Watanzania wenzangu, Ni dhahiri kumekuwa na mijadala kadha wa kadha kuhusu vyama vya siasa kuwa na vijana wao wa kuwa linda.
Nilionesha tofauti baina ya red brigade na greenguard. Wanaojitetea wakakimbilia Dictionary bila kutumia muda kufuatilia historia na chimbuko la kikundi hicho ambacho jina , matendo na malengo yake yako sawasawa na kule kilikoanzia.
Lakini mjadala mkubwa ni kuhusu mpango wa CHADEMA kuanzisha jeshi lao la chama chao, Jeshi ambalo halihitaji
msaada wa polisi wala wa Jeshi la wananchi wa Tanzania kwa mjibu wa kauli ya mkt wao mhe Mbowe. 
Ni kinyume na katiba ya nchi na hata katiba ya chama chao (pitia katiba yao). Wanavunja katiba hiyo sio kwa bahati mbaya bali ni mpango wao unawabana wa kuhakikisha amani ya nchi inatoweka . 
Jeshi wanalotaka kulianzisha si bahati mbaya,ni mpango wa siku nyingi hasa ukifuatilia walikojifunzia ideology ya Red Brigade na aliyeileta CHADEMA. 

MAANA HALISI YA RED BRIGADE NA WAANZILISHI WA HIYO TAASISI. Red Brigade ilianzia ITALIA mwaka 1970 kwa kifupi ni BR,Wanzilishi wake anafahamika kwa jina la Renato Curcio na Margherita(mara) Cagol waliokutana  wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Trento karibu na chuo alichokuwa akisoma Dr Slaa. 
Red Brigade ni kikundi kilichokuwa kinajishughulisha na kuishambulia(kudhoofisha) serikali kwa kufanya mambo mbalimbali ya Mauaji,Kuteka na Kuua wanasiasa, Kuhujumu kazi za serikali, Kuiba mali za watu, Kupandikiza chuki kati ya wananchi na serikali yao na wananchi na vyombo vya dola na Kufanya nchi isitawalike (Rejea kauli ya Dr.slaa "NCHI HAITATAWALIKA" 
Kikundi hiki kilikuwa kinatumia mwamvuli wa kuwa na uchungu na mali za umma lakini badala yake kikatumika , kuteka, kua na kumwagia sumu watu.

NOTE: Nazism ya Ujerumani chini ya Hitler ilijipambanua kama Socialist party(lakini matendo yake yalikuwa ni tofauti kabisa,Ugaidi na kuua ndio sifa yao).
Hiki kikundi kilivuma sana miaka ya 1970 hadi miaka ya 1980 (Hiki kipindi Dr.Slaa alikuwa Italia kwenye masomo na maisha yake yalikuwa huko). Red Brigade wakati huo walikuwa na kazi kubwa ya kuidhoofisha serikali iliyopo madarakani chini ya waziri mkuu Aldo Moro wakati huo.

Mwaka 1978 kilianzishwa kikundi kikubwa zaidi ndani ya RED BRIGADE(Ndio hicho chadema wanataka kukianzisha).Baada ya kuanzishwa kwa kikundi hicho kikiwa na watu 1000,kikundi hiki kilifanikiwa kumteka waziri mkuu Aldo Moro na kumuua Kinyama

Kuanzia mwaka 1974 hadi 1988 kikundi hiki kilifanya matukio ya kuteka, kuua,kumwagia sumu watu kwa matukio zaidi ya 50.Na yote haya yalilenga kufanya serikali ya Italy Isitawalike(DESTABALISE)..

KUKUA NA KUVUMA KWA RED BRIDGADE.

Matukio ya kuua na kuteka,kumwagia sumu na kuleta vurugu kila kona ya Itali kiliwafanya Red Brigade kusikika sana nakuleta hofu kwa watu.

Walikuwa wanaua na kuteka kwa USIRI mkubwa tena wakiwa wanatembea chini ya mwavuli wa chama cha kisiasa LOTTA CONTINUA na Potere Operaio.
Pia kilivuma sana kupitia Movement for Change MFC waliyoianzisha na baadaye kuipa jina la MOVIMENTO SOCIALE ITALIANO(MSI) bila shaka ndio M4C ya CHADEMA.
Ilikuwa ni miaka ya 1980 ambapo hiki kikundi kilizimwa kabisa kabisa na serikali.Serikali iliamua kuchukua hatua nzito kwa kuanzisha slogan ya ANTI-BR.

Yapo mengi sana ya kuelezea kuhusunia na kikundi hiki,(Pitia link hapa chini).

VIONGOZI WA RED BRIGADE WAKIMBIA ITALI.

Baada ya kusambaratisha Italia,RED BRIGADES wakakimbilia nchi zingine,Mfano Antonio Negri na Cesare baltisti walikimbilia France.

Wengine walikimbilia Palestina.

Takwimu zinaonesha zaidi ya watu 780 waliuawa na kumwagiwa sumu Italia chini ya BR,Lakini pia walifanya matukio zaidi ya 1400 ya uvunjifu wa amani na kuifanya Italia isitawalike.

Tafiti zinaonesha Red Brigade inaendelea kuishi kwenye nchi mbalimbali kupitia vyama vya siasa,Na moja wapo ni India,Tanzania(CHADEMA) Amerika kusini n.k

Pitia Link hii>>https://en.wikipedia.org/wiki/Red_Brigades na hiihttps://en.wikipedia.org/wiki/Red_Brigades.

ALIYEILETEA CHADEMA KIKUNDI CHA RED BRIGADE NA MABADIRIKO YA BENDERA YA CHAMA.
Wakati wote haya ya RED BRIGADE yakiendela huko Italia,Kulikuwa na Mtanzania mwenzetu akiishi na kusoma huko (mambo ya kanisa),Ni katibu mkuu wa sasa wa CHADEMA Dr.slaa, Huyu ndiye aliyeleta falsafa ya kuanzishwa kwa kikundi hicho cha kihalifu chini ya mwavuli wa chama.

Historia inatuambia Mwaka 1977 Dr Slaa alifanikiwa kupata upadirisho, Aliamua kujiendeleza kimasomo kwa kujiunga katika chuo kikuu cha Ponfical Urban Cha Roma cha huko Italia karibu na chuo walipokuwa wakisoma waanzilishi wa Red Brigade kipindi hicho Italy .

Alipokuwa Italia masomoni ndipo alipojifunza mbinu hizi za RED BRIGADE na hatimaye kuzileta CHADEMA.

Baada ya Dr.slaa kujiunga CHADEMA akaongoza ubadilishaji wa bendera ya chama (Bendera ya CHADEMA imebadilishwa na kuwekwa rangi nyekundu kama mwagaji damu Italy na aliyeasisi mabadiriko haya ni Dr.slaa akichukua sehemu ya bendera ya Red Bridgade wa Italy)na uundwaji wa katiba mpya ya chama yenye Red Bridgade(jina hili alilitoa Dr.slaa kwa kuiga lile la kikundi cha Italy) ndani.

Dr.slaa alipojiunga CHADEMA amekuwa mstari ma mbele kutengeneza mahusiano na Italia ya kisiasa

Kwa mara ya kwanza CHADEMA walipeleka vijana zaidi ya 50 kwenda masomoni Italia kujifunza mambo ya Red Bridgade kwa mwavuli wa mafunzo ya siasa na utawala.

RED BRIDGADE YA ITALIA(CHADEMA) NA KINACHOTOKEA NDANI YA NCHI YETU.

Ni wazi kabisa kabisa,Nchi yetu imekuwa ikikumbwa na mikasa ya uvunjifu wa Amani, kutekwa kwa watanzania wenzetu,Kuuawa kwa wananchi, Kutekwa na kuuawa kwa wanasiasa wenzetu kama ndago na mipango ya kuteka wandishi. 
Kubwa zaidi tumeshuhudiwa Kiongozi mkubwa wa chadema akisimama jukwaani na kujinasibu "NCHI HAITATAWALIKA"(DESTABALISE). Na kuwambia maaskofu wasiombee Amani
Ni ushuhuda ambao kila mtanzania anaweza kuusema,Mikutano inayoua niyachadema,Wanaoteka na kumwagia tindikali (sumu) ni vijana wa CHADEMA,Wanaojiita RED BRIDGADE ni CHADEMA,wanaoteka watu hao hao wanahusishwa ni CHADEMA,Chama maarufu kwa maandamano Afrika Mashariki na kati ni CHADEMA,Uvunjifu wa amani na matukio ya kigaidi yanatokea kwneye mkitano ya CHADEMA

Na hayo yote ni yale yale waliyokuwa wanayafanya RED BRIGADE wa Italia kuhakikisha serikali na chi haitawaliki.

Slogan ya MOVEMENT for Change na Peoples Power ni mwavuli tu ambao ulichukuliwa toka Magharibi kuwa ni wanademokrasia,Ili hali ni wanademogasia

Kwahiyo niseme wazi,mpango huu wanaotaka kuufanya chadema wa kuunda RB kubwa zaidi tena isiyohitaji msaada wa jeshi la polisi na Jeshi la Wa Tanzania, ni uhaini, ni ugaidi,ni maandalizi ya kupindua nchi au kuvuruga kabisa kabisa amani tuliyonayo. Kama wanavuruga amani na hii Redbrigade ndogo,itakuwaje wakiwa na jeshi.

Naunga mkono kauli ya Rais Mh.Jakaya kikwete hakuna kuundwa kwa jeshi hilo,na serikali itachukua hatua stahiki kuhakikisha nchi inafuata misingi ya katiba yake.

Hivyo basi,nawaomba watanzania tuamke, tusome nyakati kuhusiana na upinzani huu wa CHADEMA wenye mwavuli wa kisiasa kumbe ni kundi la RedBrigade wa Italy ni hatari kwa nchi yetu.
 MWIGULU  NCHEMBA,(Mbunge)



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...