Jeshi la polisi Geita linawashikilia watu wawili kwa kosa la kusambaza
ujumbe kwa njia ya simu usemao, UMEPOKEA SHILINGI 50,000.KUTOKA KWA RAIS
KIKWETE KAMA SEHEMU YA MGAO WAKO BAADA YA KIKWETE KUMUUZIA OBAMA NCHI!!
Kamanda wa polisi mkoani hapo alisema kwamba watu hao walikamatwa baada
ya kukutwa msg hizo ktk simu zao za mikononi huku wakiwa wanasambaza kwa
watu wengine.
Aliendelea kudai kua jeshi la polisi linatoa onyo kwa wale wote
wanaowachafua viongozi wa kitaifa kwa njia za ujumbe kwa simu na kwamba
watawachukulia hatua kali.
Source; Radio Free Afrika Matukio!