Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,
amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalo
fanyika Jumapili hii, Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam. Aidha, Rais atahutubia katika tamasha na pia atakuwa refa wa
mechi za wabunge wa Yanga na Simba.