Mshikemshike
kwa ajili ya Tamasha la Matumaini, Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar ambapo mastaa wa filamu za Kibongo wanaoshiriki ndondi na
wabunge, Aunt Ezekiel na Jacqueline Wolper wametamba kuwamaliza
waheshimiwa hao.
AUNT VS ESTER BULAYA
Aunt
ambaye atazichapa na Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Mara (CCM), Ester
Bulaya ameapa kuwa lazima siku hiyo ‘amuue’ mheshimiwa huyo kwa madai
kuwa kwa sasa yupo fiti baada ya kurejea kutoka kambini, Dubai.
Alisema
kuwa amepata mazoezi ya nguvu ya kurusha na kupangua ngumi kutoka kwa
mwalimu wake, Abdul Al-Mohd ambaye amempa mbinu zote za kummaliza mbunge
huyo katika raundi za mwanzo.
“Nipo
fiti sana, najua mheshimiwa Ester ni mtu wa Mara kwa wakorofi na ana
hasira lakini hilo halinipi shida, cha msingi mashabiki wangu waje
kushuhudia nikimmaliza mtu,” alisema Aunt na kuongeza:
“Ester
ni mwanasiasa mzuri na ana mazoea na majukwaa ya siasa lakini mimi
nataka niwathibitishie watu kuwa naweza kumiliki ulingo vilivyo kama
ninavyokuwa stejini.
“Kazi ni moja tu keshokutwa (Jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa, natoa tahadhari kuwa ‘nitam
uua’ mbunge wenu. Nawaahidi mashabiki wangu na watu wote ushindi ‘so’ wote tukusanyike tupate burudani na kuchangia elimu yetu.”
WOLPER VS HALIMA MDEE
Kwa upande wake, Wolper ambaye
atazichapa na Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee ametamba kuwa yupo
fiti katika kiwango chake cha juu kabisa cha mazoezi ya ndondi hivyo
anachosubiri ni kukutana na mpinzani wake ammalize.
Wolper
aliyekuwa kambini nchini Afrika Kusini akipata mbinu kutoka kwa mwalimu
wake nchini humo, alisema kwa sasa yupo fiti chini ya uangalizi wa
mwalimu wake wa muda ambaye ni mwigizaji Jacob Steven ‘JB’.
“Halima
yeye ni mwanasiasa, najua ni mtu wa maneno mengi kwenye majukwaa ya
siasa. Mimi kazi yangu ni kuigiza na kupiga ngumi hadi mtaani sasa hivi
wananiita bondia,” alisema Wolper na kuongeza:
“Mimi
ni bondia kweli. Nadhani mliniona mwaka jana nilipozichapa na Wema
Sepetu. Naomba wapigakura wa Kawe wawe tayari kwa lolote litakalotokea
kwa sababu lazima nimzimishe mbunge wao.
Tunakwenda pale kwa kazi moja tu, ‘kuwaua’ wabunge wenu.”
Hata hivyo, Wolper aliwataka mashabiki
wake na watu wote kukusanyika Uwanja wa Taifa kushuhudia ngumi za kufa
mtu na burudani nyingine kibao.
MASTAA WENGINE
Mastaa wengine watakaonyukana ni
mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema),
Zitto Kabwe ambao kila mmoja anaendelea na mazoezi mazito huku JB
akitaka kuzichapa na Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan ili ampige kwa
KO.
Katika
ndonga za ‘maprofesheno’, Mkenya Patrick Amote atanyukana na Mtanzania
Thomas Mashali huku Shadrack Muchanje wa Kenya akitoana nundu na Francis
Miyeyusho wa Bongo.