Anderson akiingia na gari yake aina ya Mercedez yenye thamani ya £168,395
Leo asubuhi wachezaji wa Manchester United walikuwa na mashindano yasiyo rasmi ya kuonyesha magari yao ya thamani wakati wakiwasili kwenye uwanja wao wa mazoezi AON Carrington. Mchezaji wa kibrazil Anderson pamoja na kutokuwa mmoja ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi sana na United - yeye ndio alikuwa mchezaji aliyekuja na gari la thamani zaidi Mercedez ambalo linauzwa kiasi cha millioni 286,271,500 za kitanzania.