Onika
Tanya Maraj maarufu kama Nicki Minaj member wa Young Money ambaye
amezaliwa miaka 30 iliyopita, anasifika kwa style yake ya kurap na jinsi
anavyojifananisha na mdoli wa barbie. Kitu kingine ambacho Nicki Minaj
anacho ni tatoo ambayo ipo kwenye mkono wa kushoto iliyoandikwa kwa
lugha ya kichina. So, umewahi kujiuliza nini maana ya tatoo ile ambayo
Nicki Minaj amejichora. Kama ulikuwa hujui ni kwamba hiyo ndiyo tatoo
pekee ambayo Nicki Minaj anayo kwenye mwili wake tofauti na boss wake
Lil Wayne ambaye karibia nusu ya mwili wake una tatoo.
Kwenye lugha ya kiingereza tatoo hile maana
yake ni ”God is always with you”, kwa kiswahili ni kwamba “Mungu siku
zote yupo pamoja nawe”. Sources zinasema kwamba Nicki Minaj mwenyewe
anasema alijichora hiyo tatoo akiwa na akili za kitoto na kama akiweza
kurudi nyuma asingeweza kuichora tena.