Ndege
iliyokuwa inambeba rais wa Somalia, imelazimika kutua kwa dharura mjini
Mogadishu baada ya moja ya mabawa yake kushika moto.
Msemaji wa Hassan
Sheikh Mohamud, alisema kuwa haijulikani kwa nini injini ya ndege
ilisita kufanya kazi. Bwana Mohamud alichaguliwa kama rais wa Somalia
mwaka jana katika mpango ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa, katika
hatua za kumaliza vita vya miaka mingi.Rais Hassan Sheikh Mohamud,
alielezea kuwa rais hakujeruhiwa lakini wazima moto walifanya kila hali
kuzima moto huo. Mwandishi wa BBC Mohamed Mwalimu, alisema kuwa magurugumu ya ndege yaliharibiwa vibaya baada ya tukio hilo. Rais alikuwa anaelekea katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, wakati ndege hiyo ilipolazimika kurejea Mogadishu. Moja ya ripoti
zilizotolewa za mwanzo kuhusu tukio hilo, ilitoka kwa akaunti ya Twitter
ya kundi la al-Shabab lakini haikusema kama imeshambulia ndege hiyo. Wanajeshi wa
Muungano wa Afrika pamoja na wale wa Somalia, wanaounga mkono bwana
Mohamud wamewaondoa wapiganaji wa al-Shabab kutoka mji mkuu Mogadishu,
mwaka jana ingawa kundi hilo bado hufanya mashambulizi ya mara kwa mara
ya kuvizia. Serikali mpya ni ya kwanza kwa zaidi ya miaka 10 kutambuliwa na serikali ya Marekani na shirika la fedha duniani (IMF).