NDEGE YA KENYA AIRWAYS IMELAZIMIKA KUTUA UGIRIKI KWA AJILI YA KUONEKANA ISHARA YA NDEGE HIYO KUWAKA MOTO.
Mtandao wa Standard Digital unaripoti kuwa ndege yenye namba
KQ117 iliyokuwa na jumla ya abiria ilitua salama katika uwanja wa
Athens kisha abiria wote na wafanyakazi wa ndege kupelekwa hotelini
kwaajili ya kupisha uchunguzi wa chanzo cha ishara ya tahadhari ya moto
katika eneo la mizigo la ndege hiyo.
Taarifa hiyo imeendelea kusema uchunguzi katika kifaa cha kugundua
dalili za moto ulifanyika ili kubaini chanzo, lakini hakuna tatizo
lolote lililoonekana.
Baada ya ukaguzi huo abiria walikuwa wanategemewa kuondoka Athens
kuendelea na safari ya Nairobi majira ya saa 11 jioni ya jana.