Mshambuliaji wa AC Milan, Mario Balotelli ametishia kununua kifaru kwa ajili ya kuwakomesha wasumbufu barabarani.
Balotelli
ambaye ni tegemeo katika kikosi cha timu ya Italia, ameweka maneno hayo
kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.
Muitaliano
huyo anayefuatiliwa na watu wapatao milioni moja ameamua kutoa
kichekesho hicho ikiwa ni sehemu ya kitisho kwa watu ambao hata hivyo
hakuwataja.
Aliweka
maandishi haya, 'When some one is driving a Ferrari and he flash you
than, just get the f*** out of the way! Pff (in case I would do the
same). 'Or maybe I should just buy a TANK!'
Halafu akaweka picha ya kifaru ambacho kinapita juu ya gari, kuonyesha atafanya hivyo kwa ambao watakuwa wasumbufu barabarani.
Balotelli
amekuwa maarufu kutokana na vituko lukuki hasa katika kipindi
alichokuwa anachezea Manchester City ya England kabla ya kuamua kuondoka
na kurejea kwao Italia.