MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia kwa dhamana Ludovick Joseph anayeshitakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatare, baada ya kusota rumande kwa zaidi ya miezi minne.
Ludovick aliachiwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa Juni 10 mwaka huu.
Washitakiwa hao waliofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 18 mwaka huu, wanakabiliwa na shitaka la kutaka kumdhuru Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky kwa kutumia sumu.