Wakati
nikiwa Tunduru nilipata simulizi mbalimbali kuhusiana na wilaya hiyo
jinsi ilivyo tajiri wa ardhi yenye rutuba ya kutosha pamoja na maji
mengi ya kutosha kulinganisha na wilaya nyingine zilizopo mikoa ya
Kusini.
Lakini
kilichonisisimua zaidi ni simulizi juu ya hili bwawa ambalo hata
kuletwa na kufika hapa na mwenyeji wetu ilikuwa shughuli kidogo na
ilitulazimu tuwaombe wenyewe ili tufike na kurudi salama. Unaweza
kulidharau kwa macho ukilitazama lakini amini usiamini ninachokueleza
ndicho nilichoshuhdiwa na wenyeji. Bwawa hili lina nguvu za ajabu ambapo
kama utakuwa umekwenda kwa shughuli zako na kuhatarisha matumizi yake
ikiwa ni kukojoa, kutukana matusi na mambo mengine ambayo ni chukizo,
hakika unapoteza maisha. Na inasemekana kila baada ya kipindi fulani mtu
hupoteza maisha kwa kufia humo bwawani.Bwawa
hili lililopo Kiuma wilaya ya Tunduru linasemekana linatoa maji safi ya
kunywa pamoja na matumizi mengine ikiwamo ufyatuaji wa tofali za udongo
kwa wenyeji. Mwaka jana wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kiuma
iliyopo karibu na bwawa hilo walikwenda kuoga pamoja na kufua nguo
lakini mmoja wao hakurudi salama.Ilikuwaje?
Inaelezwa kwamba mara baada ya kijana huyo kumaliza shughuli zake
alikaa pembeni ya bwawa akiwasubiri wenzake. Lakini kadiri jua
lilivyozidi kuongezeka alihisi joto na kuonelea ni busara akaingia
bwawani ili apooze joto la mwili wake. Wakati akiwa bwawani kijana huyo
alitamka lugha ya matusi na maneno mabaya kuhusu maji ya bwawa hilo
ghafla akahisi nguvu kali ikimvuta kuelekea chini. Akaomba msaada kwa
wenzake ambao walijaribu kutaka kumwokoa wakaona nawao wanazidiwa nguvu
kwa kuvutwa ikashidnikana na mwenzao akatokomea majini.Baada
ya mwenzao kutokomea majini, vijana wale walikwenda kutoa taarifa
shuleni kwao kwamba mwenzao amepotea katika maji bwawani na wamejaribu
kumwokoa wakashindwa. Wakuu na wahusika wengine wakaanza taratibu za
uokoaji ili kusalimisha maisha ya kijana huyo ikiwa na Mkuu wa kituo cha
Kiuma kuagiza ndege binafsi yenye wataalam wa uokoaji kutoka Dar es
salaam kuja mara moja kumwopoa kijana huyo jitihada ambazo
zilishindikana pamoja na waokoaji wengine. Ndipo ikalazimu kwenda kwa
wazee wa jadi ambao walifanya tambiko na kuomba kwa muda wa siku 3 na
mara baada ya hapo kazi ya kumwopoa ikaanza. Inaelezwa kwamba kijana
huyo alipatikana lakini nguvu ya ziada ilitumika kwani mbali na
kupatikana kwake lakini bado walinyang'anyana wakiwa majini. Alipoopolewa
kijana huyo alikuwa tayari amekwishafariki cha ajabu kilichoonekana ni
kutokwa na damu puani kwa kijana huyo hali alikuwa majini kwa siku 3.
Tukio hilo lilileta simanzi kubwa katika jamii nzima ya Kiuma na uongozi
wa Kiuma ulichukua hatua ya kuwapiga marufuku wanafunzi wake kufika
katika eneo hilo.Walioingia
kumwokoa kijana huyo walieleza kwamba walikutana na vitu ambavyo ni
adimu kuonekana katika hali ya kawaida katika maisha ya binadamu. Ikiwa
na sehemu ambazo hakuna maji kabisa na kuwa kukavu kama nchi kavu huku
upande mwingine maji yakiwa yamezunguka pamoja na matukio mengine ya
ajabu ambayo ni ngumu kumuelezea mtu akaamini.Inaelezwa
kwamba kuna bwana mmoja mvuvi alikwenda kutafuta kitoweo bwawani hapo
alipotwika ndoano na kuvuta akavuta lundo la samaki wakavu waliochomekwa
katika umambo mmoja jamaa akatimua mbio na ikawa mwanzo na mwisho wa
kukanyaga hapo. Matukio mengine ni kama kukuta nguo zimeanikwa na
wahusika hawaonekani ama kusikia sauti za watu zikiongea na usiwaone.