Baada ya malalamiko hayo kuzifikia mamlaka zinazohusika za jiji la Los Angeles, Brown aliamrishwa aufute mchoro huo kitu ambacho alikipinga kwa madai kuwa sheria zinamlinda. Baada ya mvutano wa tokea (May) kati yake na mamlaka ya jiji hilo hatimaye leo (July 12) wafanyakazi wameonekana wakiupaka rangi ukuta huo na kufunika mchoro huo.
Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa uamuzi wa kufuta Graffiti hiyo ni wa Chris mwenyewe na sio amri ya jiji la Los Angeles.
Idara ya ujenzi ya Los Angeles imesema endapo mpaka kufikia kesho wataridhishwa kuwa mchoro huo umefutika kabisa, wataifuta fain ambayo ilikuwa apigwe Breezy kwa kuweka mchoro bila kupata vibali.