Mabeste ajibu swali muhimu lililokuwa likiumizwa vichwa vya wengi
Rapper
wa B’Hits, Mabeste leo ametoa fursa kwa mashabiki wake kumuuliza
maswali kupitia ukurasa wa Facebook. Miongoni mwa maswali muhimu
yaliyoulizwa na ambayo watu wengi wamekuwa wakijiuliza pia ni pamoja
kuhusu uraia wa wazazi wake na shughuli anayoifanya zaidi ya muziki. Akijibu swali kuhusu wazazi wake, Mabeste Venance amesema baba yake ni Mtanzania huku mama yake akiwa Mkenya. Pia amesema licha ya kufanya muziki, amekuwa akijihusisha na biashara
na kwamba wimbo wake ujao baada ya ‘Dole’ unaitwa Are You Like Now’