Waziri
wa Ardhi Makazi Maji na Nishati Ramadhani abdalla Shaabani
---
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar
Waziri
wa Ardhi Makazi Maji na Nishati Ramadhani abdalla Shaabani amesema
Jumla ya hati 344 zimetolewa katika maeneo mbali mbali ya Unguja na
Pemba ambapo hati 35 kwa ajili kilimo na 309 kwa ajili ya makazi.
Hayo
ameyasema leo huko Baraza la wa kilishi wakati alipo kuwa akisoma kitabu
chake cha bajeti ya Wizara hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi
kwa mwaka wa fedha 2013-2014 mwaka ujaoAmsema
ametoa hati hizo kwa kuwapa fursa wananchi kuwapatia makazi na
kuimarisho kilimo ikiwa ni sehemu ya uendelezaji maisha ya mwanadamu
akiwa hai.
Amesema
muendelezo wa utoaji wa hati hizo pia ulifuatana na zoezi la
kubadilisha hati za zamani na kuwapatia wananchi hati mpya za kisasa
na kupokea hati za zamani 105 na kubadilishwa kwa kuwapa wahusika hati
mpya .
Aidha
waziri huyo akielezea malengo yao kwa mwaka huu wa fedha ni pamoja na
kuimarisha mfumo wa utoaji taarifa za wizara na kusimamia utekelezaji
wakazi za wizara kwa ufuatiliaji na kutathimini miradi kumi ya maendeleo
ambayo ni pamoja na ,usambazaji wa maji na usafi wa mawzingira .
Nyengine
kuimarisha mradi wa mindo mbinu ya maji mkoa mjinimagharibi na
kuijengea uwezo mamlaka kifedha ,na uhuwishaji na upanuzi shghuli za
maji mijini na vijijini .
Pia
kusambaza umeme vijijini,uimarishaji wa miundo mbinu ya umeme unguja na
pemba ,ufungaji wa mita elfu 20 za tukuza, utekelezaji sera ya nishati
,utafiti nishati mbadala, usimamizi endelevu wa aridhi na mazingira
Vilevile
kukuza kuimarisha uhusiano baina ya Wizara tatu za SMT na washirika
wa Maendeleo na kuratibu matayarisho ya sera ya mipango miji na
kukamilisha mapitio ya sera ya ardhi na sera mbali mbali za wizara