Raia mmoja mkazi wa Mwinilunga nchini Zambia ameponea chupu chupu kufa baada ya kuvamiwa na chatu.
Kelvin
Katoka ambaye ni dereva wa malori yanayochimba mchanga katika machimbo
ya Copa alirukiwa na chatu huyo mkubwa na kuanza kumzungurusha kwa nia
ya kuanza kummeza mzima mzima.
Hata
hivyo, Kelvin alipambana na chatu yule kwa kumng'ata sehemu mbali mbali
za mwili wa ke bila mafanikio. Hapo Kelvina mwenye umri wa miaka 25 tu
alijitahidi kuchomoa kisu mfukoni na kumchoma joka huyo mara kadhaa
kabla hajaishiwa nguvu na kupoteza fahamu wakati ambapo bado chatu yuke
alikuwa ameshinda na kumminya na kuanza kummeza.
Kelvin
akishahis mate ya nyoka yulekichwani ndipo wafanyakazi wenzake wawili
walipopita katika eneo lile na kumuua nyoka yule na kumkimbiza Kelvin
Hospitalini. Kelvin anaendelea vizuri na matibabu.