.
MWANARIADHA
nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica, Usain Bolt ametuma ujumbe kwa
wapinzani wake baada ya kufanikiwa kushinda mbio za mita 200 za Diamond
League zilizofanyika jijini Paris kwa kutumia muda wa sekunde 19.73
ukiwa ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Bolt ambaye anashikilia
rekodi ya dunia katika mbio hizo alifabnikiwa mbio kirahisi na kuuzidi
muda wa haraka zaidi uliowekwa kwa mwaka huu na Tyson Gay wa Marekani
mwezi mmoja kabla ya mashindano ya riadha ya dunia yatakayofanyika
jijini Moscow, Urusi. Akihojiwa mara baada
yam
bio hizo Bolt amesema anajisikia vyema kwa kushinda mbio hizo lakini
bado bado ana kazi ya kufanya kuhakikisha anakuwa katika kiwango chake
ifikapo michuano ya dunia. Nafasi ya pili katika mbio hizo ilikwenda kwa
Warren Weir wa Jamaica aliyetumia muda wa sekunde 19.92 huku nafasi ya
tatu ikienda kwa Christophe Lemaitre wa Ufaransa aliyetumia muda wa
sekunde 20.07.