
MMILIKI
wa Kampuni ya Filamu ya Endless Fame, Wema Sepetu hivi karibuni
amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya majirani zake kumshitaki kwenye
serikali ya mtaa kufuatia tabia ya wafanyakazi wake kutiririsha maji
machafu mtaani.
Taarifa
iliyolifikia inadai kuwa, majirani wa Wema katika eneo analoishi,
Kijitonyama jijini Dar wamekuwa wakimlalamikia msanii huyo kwa kitendo
hicho lakini imeonekana uvumilivu umewashinda.
“Mara
kwa mara wafanyakazi wake wamekuwa wakitiririsha maji hapa mtaani sasa
leo tumeona tukamshitaki serikali za mitaa ili sheria ichukue mkondo
wake,” alisema mmoja wa majirani wa staa huyo aliyeomba jina lake
lisiandikwe .
Juni
26, mwaka huu Ijumaa lilifika kwenye nyumbani kwa Wema na kushuhudia
maji yakitoka kisha kuzagaa mtaani na muda mfupi baadaye alifika Afisa
Mtendaji wa Kata ya Makumbusho (jina halikufahamika mara moja) ambaye
aligonga kwenye nyumba ya Wema, baada ya muda alitoka binti wa kazi
aitwaye Bite.
Katika
mazungumzo yao, Bite alionekana kujitetea lakini baadaye ilibainika
wana makosa na akatakiwa kwenda ofisi za kata kwa maelezo zaidi.
Amri
hiyo ilionekana kuwa ngumu kwa Bite na wafanyakazi wenzake ambapo
busara zilitumika na kiongozi huyo wa serikali akataka walipe faini na
kuwaonya waache tabia hiyo.
Kufuatia
hatua hiyo, Bite aliingia ndani (inadaiwa alikwenda kumtonya Wema)
ndipo alipotoka akiwa na fedha ambazo Ijumaa halikujua ni kiasi gani,
wakasainishana kisha mchezo ukaishia hapo.
Jitihada
za kumpata Wema kuzungumzia sakata hilo ziligonga mwamba kutokana na
msanii huyo kutopokea simu na hata mwandishi alipofika nyumbani kwake
aliambiwa hayupo.



