Josephine Michael akiwa barabarani baada ya kujifungua.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa baada ya Josephine kujifungua salama mtoto wa kiume.
Mmoja wa akina mama waliofika eneo hilo akiwa amembeba mtoto wakati mama yake akihojiwa na mwanahabari.
Wananchi waliofika eneo hilo wakiwa na Josephine (aliyekaa chini).
Na Dustan Shekidele, Morogoro
BINTI
mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo
ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani
wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.
Tukio
hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha
Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.
Mwandishi
wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha
usalama barabarani ‘trafiki’ (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya
kuongoza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo
akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto
wa kiume ‘dume la nguvu’.
Awali, wanawake hao walizungusha kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao alipokuwa akijifungua.
Mara
baada ya zoezi hilo kwenda salama, Josephine alisema alipatwa na
uchungu alfajiri ya siku hiyo na mume wake aliwapigia simu madereva wa
teksi zaidi ya wawili ambao waligoma kufika kijijini kwao kutokana na
ubovu wa barabara.
“Hali
ilipozidi kuwa mbaya tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye alifika
na kunibeba huku mume wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli yake,”
alisema Josephine kwa uchangamfu.
Binti
huyo alisema kwamba walipofika eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya
akashindwa kujizuia baada ya mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba
dereva wa bodaboda asimame ndipo alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa
mbaya.
Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi alipojifungua salama.
Dereva
wa bodaboda aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo
Shilagi alikiri barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.
SOURCE: GPL







