Wakali wa
bongo fleva wenye vocal zenye ladha na nguvu ya aina yake Lady JayDee
‘Anaconda’ na Q-Chillah, wamekutana tena studio kurekodi wimbo mpya
ikiwa ni miaka kadhaa imepita walipotisha na wimbo wao ‘Zamani’.
Lady JayDee
alipost picha kupitia akaunti yake ya Twitter ikimuonesha yeye na
Q-chilla wakiwa ndani ya studio za Combination sound na Man Walter, na
kuisindikiza na maelezo.
Hakuchelewa kutaja jina la wimbo huo “Sukari” na kuonesha kuikubali sana, hii inatoa picha kuwa kitu kikubwa kinakuja.
“Sukari - Qchillah & Jide another hit ??? ☺ #Justasking.” Aliongeza.
Tuisubiri hiyo sukari tuonje ladha yake kwa masikio.




