|
Jailo
Rashid (30), Niza Hamis (24) na Medi Keya(33) ambao kwa pamoja
wanadhaniwa kumuua kwa maksudi, Ambrose Shayo(45) aliyekuwa ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Saccos Taifa na Tazara SACCOS ya Jijini Mbeya. |
Hili ndilo eneo alilouwawa mwenyekiti huyo wa SACCOS
|
Hili ndilo gari alilokuwa amepanda Mwenyekiti wa
Chama cha kuweka na Kukopa (Saccoss)
WATU
watatu wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutenda kosa la kumuua kwa
kukusudia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha kuweka na Kukopa (Saccoss),
Mbeya
Akisoma
mashtaka hayo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali Hebel Kihaka mbele ya
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya Venance Mlingi alidai
Watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa la mauaji kwa maksudi kinyume
cha Sheria ya Makosa ya Jinai kifungu cha 196 sura ya 16 kama
ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Jailo Rashid (30), Niza Hamis (24) na Medi
Keya(33) ambao kwa pamoja walimuua kwa maksudi, Ambrose Shayo(45)
aliyekuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Saccos Taifa na Tazara Saccos ya
Jijini Mbeya.
Alisema
watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo April 20, Mwaka huu
majira ya saa 3 usiku katika Kijiji cha Itagano Kawatere Jijini Mbeya
ambapo Marehemu alivamiwa na watu hao kisha kumuua.
Kwa
upande wake Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Venance Mlingi alisema Kwa
mujibu wa Sheria watuhumiwa hawaruhusiwi kujibu chochote kutokana na
Mahakama yake kutokuwa na uwezo wa kusikiliza Shauri la Mauaji.
Aliongeza
kuwa Shauri hilo limeletwa kwa ajili ya hatua za awali ambapo baada ya
upelelezi kukamilika litapelekwa Mahakama kuu kwa ajili ya taratibu za
kusikiliza, pia aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 3, Mwaka huu
itakapotajwa tena.
Na Mbeya yetu
|