Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali Schwarzenegger mwenye miaka 65 alitoa taarifa hiyo huko Australia hivi karibuni alipohudhuria mkutano wa ‘21st Century Financial Education Summit’, “I’m very happy that the studios want me to be in ‘Terminator 5′ and to star as The Terminator, which we start shooting in January”, alisema.
Patrick Lussier na Laeta Kalogridis ambao ni marafiki wa muanzilishi wa movie ya ‘Terminator’ James Cameron ndio wamepewa deal ya kuandika script ya movie hiyo na kampuni ya Paramount ndio imekuwa katika mazungumzo kwaajili ya kusambaza movie hiyo.
Hii itakuwa ni mara ya 4 kwa Schwarzenegger kushiriki katika movie hiyo baada ya kushindwa kushiriki katika Terminator 4 kutokana na majukumu ya u- Governor wa California kwa wakati inatengenezwa.
Kwa mara ya kwanza Temrminator ilianza kuonekana mwaka (1984), na kufuatiwa na Temrminator 2 iliyotoka mwaka (1991), Terminator 3 ilitoka (2003) na Terminator 4 (2009).