Kupitia Instagram, Peter Okoye ambaye ni mmoja wa mapacha hao, ameweka picha aliyoiandikia: It’s a WORLD MUST WATCH VIDEO. Out in less than 24hrs. #Personally.
Baada ya kukaa kimya kwa muda bila kuachia video mpya, kundi la mapacha wa Nigeria, P-Square, saa kadhaa zijazo litaachia video na wimbo mpya, ‘Personally’.
Wakati huo huo, P-Square ikiwa na bendi ya watu 12 itaanza ziara ya Marekani na Canada hivi karibuni ambapo tarehe za ziara hiyo zitatangazwa wiki ijayo.