Kwa wasiomfahamu wanaweza kudhania kuwa mwanamitindo huyo ni raia wa Italia kwa uzalendo aliouonyesha akiwa uwanjani lakini yeye ni raia wa Ubelgiji . Uwepo wa Fanny uwanjani unaonekana kumsaidia Super Mario ambaye alifunga moja ya mabao yaliyoisaidia Italia kushinda 4-3.
Hivi karibuni Mrio alimvika mpenzi wake Fanny pete ya uchumba yenye thamani ya paundi laki moja baada ya tetesi kuwa zimesikika juu ya wawili hao kuachana kwenye mataa.