Vibao vya matangazo vilivyozagaa
nchini vikitangaza huduma kutoka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji,
havidanganyi. Vinadhihirisha ukweli kuwa wapo wateja wanaohitaji huduma
hiyo kwa wingi.
Aina za dawa
Mfano dawa za kumlinda mume ziko za
aina mbili, zinazofanya kazi ya kumkosesha nguvu ya kufanya tendo la
kujamiiana anapokwenda kwa hawara na zile ambazo humfanya moyo uwe mzito
kusaliti ndoa.
Uchunguzi wa gazeti hili katika viunga
vya Jiji la Dar es Salaam ulibaini kuwa katika kila vibao kumi vya
matangazo, vinane vilitaja huduma ya kumtuliza mpenzi, mume au mke.
Ilibainika kuwa waganga wengi wa
kienyeji, wanatoa dawa za mapenzi kuliko hata zile za kupandisha cheo,
kutoa mikosi au za bahati.
Mganga mmoja, kwa jina la Bibi
Maajabu, alisema wateja wake wengi ni wanawake ambao hufika kumwona kwa
ajili ya kupata dawa za kumdhibiti mume.
“Wengi wanafika hapa wanaomba dawa za
kumdhibiti mume, wanaume wanaokuja kwa ajili ya kuwadhibiti wake zao si
wengi kama walivyo wanawake,” alisema Bibi Maajabu ambaye anapatikana
maeneo ya Njia Panda ya Kigogo.
Alisema yeye anatoa dawa kwa wanawake hao, dawa ambazo hata hivyo anadai ni siri yake na wateja wake tu.
Bibi huyo alisema dawa zake zinafanya kazi kweli na wala hakuna utapeli kama wafanyavyo waganga wengine.
Mganga mwingine, mkazi wa Tandale
maarufu kwa jina la K, yeye hakutofautiana na Bibi Maajabu. Alisema
wateja wake wakubwa ni wanawake hasa wenye matatizo ya ndoa na hufika
kwake kutaka kupata ‘mwarobaini’ wa kumdhibiti mume. ...Soma zaidi;
http://www.mwananchi.co.tz