SIKU moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutoa
ruksa kwa Jeshi la Polisi kutembeza kipigo kwa wanaokaidi amri, baadhi ya
wanasiasa wamelaani na kusema inachochea ukatili na kuvuruga amani ya nchi.
Wakizungumza Dar es Salaam jana na MTANZANIA walisema kauli hiyo imebeba ujumbe
mzito wa hatari wenye dhana na tafsiri tofauti ambayo itasambaratisha uhusiano
uliopo kati ya raia na polisi.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, alisema kauli ya Pinda imekiuka sheria na kukiuka misingi ya haki za raia.
“Kutokana na kauli ya Pinda inaelekeza kwamba polisi wapige raia kadri ya uwezo wao, hii ina maana tayari Serikali imetoa kibali kwa jeshi hilo kuua, kufanya unyama wa aina yoyote ile.
“Inadhihirika wazi sasa polisi wamepewa kibali cha kupiga raia na viongozi wale wanaoipinga CCM na Serikali yake, itakuwa tayari kuwalinda popote pale hata katika vyombo vya sheria.
“Pia kauli ya Pinda imetoa ruksa kwa polisi kuendelea kufanya ukatili na hii inaonyesha wazi yale matukio yaliyowahi kutokea yakiwamo ya waandishi wa habari, wanachama wa vyama vya siasa, viongozi wa dini na vyama yalikuwa na baraka ya Serikali na ndio maana hadi sasa hatua hazijachukuliwa.
“Binafsi nimeshangazwa na kauli hiyo ambayo tena imetaja maeneo ambayo tayari kulitokea vurugu ambapo raia walipigwa na kuuawa na polisi, bila uficho Pinda ametaja vurugu za Mtwara na Arusha, pia alisema kwamba Serikali imechoshwa na vurugu hizo na kilichobaki ni kupiga,” alisema Mtatiro.
Alisema hatua hiyo iliyochukuliwa na Pinda itasababisha uvunjifu wa amani kwa kuwa raia wataendelea kuchukia polisi na kuleta uhasama ndani ya jamii.
Naye, Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA), ambaye amelazwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), alisema pengine kauli ya Pinda ilitokana na msukumo wa hisia.
“Binafsi sikutarajia kauli kama ile kutoka kwa Pinda kwa sababu mnajua kasomea sheria, pengine aliathirika na matukio yaliyotokea.
“Kuna wakati kiongozi anaweza kukosea na kutamka jambo hakulitegemea, isitoshe Pinda alitoa kauli hiyo wakati akiwa kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa hapo, labda tutarajie kuomba samahani.
“Kama kweli kauli yake itaachwa na polisi kuitekeleza tutarajie machafuko na chuki kati ya wananchi na polisi na pengine kushindwa kuishi uraiani kwa kuhofia usalama,” alisema Nassari.
Pinda alitoa kauli hiyo juzi wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), aliyetaka kujua mipango ya Serikali iliyopo katika kubaini kiini cha vurugu zinazoendelea kutokea nchini badala ya kuelekeza shutuma kwa wanasiasa.
Chanzo: MTANZANIA