
Mzee
Charles Magali ambae hivi karibuni amekuwa akionekana Mjini Dodoma na
Waheshimiwa na amekili kuwa na mpango wa kugombea ubunge Jimbo lolote la
Morogoro.

Nguvu
ya wasanii imeendelea kutikisa viongozi wa kisiasa na sasa kila chama
kina mpango wa kuwashawishi wasanii hao kutangaza nia kwenye majimbo
wanayokuwa wanakubarika,ambapo msanii nyota nchini na kipenzi cha watu
Mzee Charles Magali amesema yuko tayari kugombea jimbo lolote endapo
atatakiwa kufanya hivyo.
Akiongea
na mwandishi wetu kwa njia ya simu toka mjini Dodoma msanii huyo
alisema kuwa yuko kwenye mazungumzo mbalimbali na waheshimiwa Wabunge na
Mawaziri na kuonekana kwake ndani ya bunge kuna mambo mengi ikiwemo
alikuwa akifatilia kuwakilishwa kwa baje ya nchi.
Aidha msanii huyo aliongeza kusema "
Mimi ni Chama tawala yani CCM hivyo nina maamuzi yangu binafsi ya
kuamua kama nahitaji kugombea ubunge au laa hivyo kama chana kitahitaji
nifanye hivyo nitafanya haraka sana na napenda kugombea Mkoani kwangu
kwa vile bado nina kiu ya kuuletea mkoa wangu maendelea zaidi ya haya
yaliyopo" Alisema Mzee Magali.