Na.Mo Blog Team
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeendelea na operesheni
mbalimbali kwa mafanikio, ikiwemo kukama wahalifu, kuokoa mali
zilzoibiwa na kuwadhibiti madereva wanaokiuka sheria za barabara.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kamishna wa Polisi
Kanda Maalum Dar es Salaam Suleiman Kova (pichani) amesema jeshi hilo
limefanikiwa kuwakamata majambazi wanane hatari wanaojihusisha na
uporaji wa mali za raia wa kigeni ufukweni mwa bahari ya Hindi (Coco
Beach).
Pia
Kamanda Kova amesema Jeshi hilo limemkamata mtunza bustani aitwaye
Philemon Laiza mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa Mikocheni B maeneo ya
nyumba za serikali anayefanya kazi nyumbani kwa Jaji Kileo, akituhumiwa
kuhusika na mauaji ya Perpetua mainab (30) mtumishi wa ndani raia wa
Kenya aliyekutwa amekufa baada ya mwili wake kuchinjwa sehemu ya shingo,
jeraha mkono wa kushoto karibu na kiganja na jeraha kwenye paji la uso.
Katika
tukio lingine, Jeshi hilo limefanikisha kuokolewa kwa mali ya Wachina
(Power Tiller) zenye thamani ya Tsh. 157,000,000/= ikiwa ni pamoja na
kumkamata tapeli hatari Satara Emmanuel (42) aliyeitapeli kampuni ya
AFRICATIC iliyopo Nyerere Road kwa kuonyesha nyaraka za kugushi kwamba
ameshinda zabuni ya ununuzi wa Power Tiller katika Halmashauri ya Mbulu
hali akijua anadanganya.