Maajabu ya uumbaji yamemfanya mama mzazi wa Xiao Wei ambaye ni
mchina amwage machozi akiomba msaada wa kunusuru maisha ya
mwanae mwenye umri wa miezi 7 aliyezaliwa na makalio matatu...
Kalio la tatu lipo kama mkia mfupi, wenye urefu wa sentimita 8 ( 8 cm ), katikati ya makalio mengine mawili.
Akiongea kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo amedai kuwa kwa
muda mrefu amekuwa akiwaomba madaktari wafanye upasuaji wa
tako hilo lakini wao wamekuwa wakimjibu kuwa hiyo si kazi
nyepesi kama anavyodhani....
"Tukilikata litaota tena, hivyo hatutakiwi kukurupuka na badala
yake tutakiwa kupata muda wa kupitia vitu vingi ukiwemo mrija
wa uti wa mgongo ambapo kalio hilo limejiegesha"