Lejendari
wa soka raia wa Brazil, Pele, anaamini kuwa kurejea kwa kocha mwenye
maneno mengi, The spesho Jose Mourinho katika klabu yake ya zamani ya
Chelsea ya jijini London ni chagua sahihi kwa klabu hiyo.
Mashabiki
wengi wa klabu ya Chelsea wanaamini kuwa kurejea kwa Mourinho darajani,
mataji ya ligi kuu yatarejea tena klabuni hapo kama miaka ya 2005 na
2006.
Ingawa
Pele anakubaki maamuzi ya Roman Abramovich kumrejesha Mourinho, lakini
ameonya kuwa kurejea kwa kocha huyo sio sababu ya kutegemea mafanikio
makubwa.
Pele mwenye umri wa miaka 72, ameimbia televisheni ya CNN kuwa kurejea kwa Mourinho katika klabu ya Chelsea ni jambo zuri kwani ni kocha bora.
“Ni
kocha mwenye kipaji kikubwa na mkweli. Najua sana. Lakini soka lina
maajabu yake. Ana bahati sana katika kazi yake, wakati mwingine kizuri
huwa hakifanikiwi”. Alisema Pele.
Amerudi mjini: Pele amesema Chelsea imefanya maamuzi sahihi kumrejesha Mourinho darajani
Pele Mpya: Nyota wa Barcelona Neymar, mwenye umri wa miaka 21, amewavutiwa wengi na kutajwa kuwa Pele mpya wa Brazil.
Wiki hii
pia habari kubwa wiki hii ni Neymar kutimka katika klabu ya Santos ya
Brazil, klabu ambayo Pele alicheza na kuifungia mabao 589 katika michezo
605 kuanzia mwaka 1956-1974.
Neymar
ameifungia Santos mabao 54 katika mechi 103 na sasa anatajwa kuwa Pele
mpya wa Brazil, lakini kwa upnde wake Pele anakataa kumfananisha na
kinda huyo wa dunia.
Pele
amekataa kulinganishwa na bwana mdogo Neymar, lakini amekiri kuwa
kijana huyo ni moja kati ya wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea nchini
Brazil
Pele alisema ” Neymar kuwa kama Pele mpya ni jambo gumu sana kwa sababu mama yangu na baba yangu walishamaliza kazi ya kuzaa”.
Pele aliendelea kueleza kuwa hakuna shaka kabisa kuwa Neymar ni moja kati ya vipaji vikubwa nchini Brazil.
“Kiukweli
Brazil vipaji vingi vimewahi kutokea kama Zico, Tostao, Rivelino, Pele,
Ronaldinho, lakini kwa miaka miwili iliyopita, Neymar ana kipaji
kikubwa zaidi”. Alisema Pele.