Mkuu
 wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magesa Mlongo  akiwakaribisha Wajumbe kwenye 
 Mkutano Mkuu wa  Mwaka wa Kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji 
Vijijini, jijini humo. wananchi
 wa vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na kuweka mikakati ya 
kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji huo.  
 
Waziri
 wa Maji Prof. Jumanne Maghembe (Mb)  akihutubia wajumbe (hawapo  
pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa 
Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji  Vijijini, 
unaojadili utekelezaji wa kuwapatia  
 
Waziri
 Mkuu Mizengo K. P. Pinda  akihutubia wajumbe (hawapo  pichani) wakati 
wa ufungunzi wa Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji  
Vijijini, Jijini Arusha unaojadili utekelezaji wa kuwapatia wananchi wa 
vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na kuweka mikakati ya 
kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji huo. 
 
Wajumbe
 wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Mhe.  Mizengo K. P. Pinda  hayupo 
pichani wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa 
Miradi ya Maji  Vijijini, Jijini Arusha unaojadili utekelezaji wa 
kuwapatia wananchi wa vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na 
kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika 
utekelezaji huo.
Waziri
 Mkuu Mizengo Pinda amefungua Mkutano Mkuu wa Kujadili Utekelezaji wa 
Miradi ya Maji Vijijini, jijini Arusha mwanzoni mwa wiki hii. Mkutano 
huu unalenga kujadili changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa 
programu katika mwaka 2012/2013 na namna ya kuzikabili changamoto hizo.
Akifungua
 mkutano huo, Waziri Mkuu aliagiza Halmashauri zote kukamilisha ujenzi 
wa miundombinu ya maji kwa vijiji 10 na ujenzi wa miradi ya maji 
inayoleta matokeo ya haraka katika kipindi cha mwaka 2012/13 na 2013/14.
Waziri
 Mkuu alisisitiza kuwa mwelekeo na malengo ya mkutano huu uwe ni kujenga
 mkakati endelevu wa kutoa huduma ya maji kwa kuzingatia mahitaji ya 
kiuchumi na kijamii hususan wananchi walioko vijijini kwa lengo la 
kuwaondolea adha kubwa ya ukosefu wa maji. 
“Hili
 linawezekana kama kila mmoja wenu anatimiza wajibu wake kwa bidii, 
maarifa, juhudi na nidhamu ya hali ya juu, nawakumbusha kuwa, jukumu 
mlilopewa na taifa ni kubwa na muhimu sana.” Alisema Waziri Mkuu.
Waziri
 wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua 
Mkutano huo, aliwataka washiriki kutekeleza jukumu la kuwapatia wananchi
 washio vijiji huduma ya maji kwa kutumia fedha zinazotolewa kwa ajili 
ya kutekeleza miradi.
“Fedha
 tunazopewa ni za wananchi, na ni lazima tuweze kueleza kila shilingi 
iliyopokelewa imefanya kazi gani ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji”. 
Alisisitiza Waziri Maghembe.
Mkutano
 huu umeanza tarehe 3 hadi tarehe 7 Juni 2013, na mada mbalimbali 
zitawasilishwa ikiwa ni pamoja na yaliyojitokeza katika ufuatiliaji wa 
miradi ya maji nchini kwa mwaka 2012/2013, mpango wa utekelezaji wa 
miradi ya maji kwa mwaka 2013/2014.
Nyingine
 ni Utekelezaji wa Kampeini ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira, 
yaliyojitokeza wakati wa kupitia Mfumo wa Kiteknolojia wa Kutoa Taarifa (MIS),
 kila mkoa utatoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa miradi ya maji 
kwenye vijiji na miradi mingine ya maji, mfumo wa ufuatiliaji wa kikanda
 na mapitio ya usanifu wa miradi ya maji. 
Washiriki
 wa mkutano huu wanajadili namna ya kuongeza kasi ya Utekelezaji wa 
Mpango wa Mwaka 2013/2014 ikizingatiwa ni mwaka wa kwanza wa Utekelezaji
 wa Mpango Mpya wa Kuleta Matokeo ya Haraka Sasa (Big Result Now). Ambapo baada ya majadiliano washiriki wataingia mkataba wa kiutendaji (Performance Agreement) kati ya Halmashauri na Mkoa na kati ya Mkoa na OWM – TAMISEMI. 
Mkataba
 huo utakuwa na majukumu ya kila mtekelezaji na hatua anayotakiwa 
kufikia katika kipindi cha mwaka 2013/2014 kwa kufuata viashiria 
vilivyowekwa kitaifa. 



