Mtoto huyo aliyeokotwa huko katika mtaa wa mlandege saa mbili asubuhi amekutwa tayari akiwa ameshafariki ila polisi wanamshikilia mama mmoja ambaye jina lake halikupatikana hadi tunaingia kuziandika habari hizi,polisi wamelazimika kumkamata mwanamama huyo kufuatia kauli za majirani wakimtuhumu kuwa huyo mtoto ni wake kwani alikuwa na mimba na ghafla haipo na pia uchunguzi unaonyesha kuwa ni kama anauhusika japo bado polisi hawajatowa tamko kufuatia mahojiano hayo japo waandishi wa thesuperstarstz waliopo huko iringa walifika eneo husika na baadae polisi lakini walijibiwa kuwa wasubiri hadi uchunguzi ukamilike.
Ama kwa hakika ile kauli ya ubinadamu kazi wala walioileta hawakukosea
maana kwasasa binadamu tumegeuka wanyama zaidi ya wanyama wenyewe,kauli
hii inakuja kufutia tukio la ajabu limetoke mjini iringa na kuvuta hisia
za watu waliokuwa katika eneo hilo kushuhudia kichanga hichi
kisichokuwa na hatia kikiokotwa eneo la jalalani.
Mungu ailaze roho ya kichanga huyu mahali pema peponi amini