Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Friday, June 7, 2013

KAMANDA MKUU WA POLISI MKOANI DODOMA AWAANGUKIA VIONGOZI WA DINI

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akizungumza na viongozi wa madhehebu ya dini ofisini kwake alipowaita ili kujenga mahusiano ya kimawasiliano.(Picha na John Banda)

Na John Banda,Dodoma.

 JESHI la Polisi Mkoani Dodoma imewaomba viongozi wa madhehebu ya dini kushirikiana katika mawasiliano ili kubaini uhalifu na wahalifu.
Ombi hilo limetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa David Misime, alipokuwa akizungumza na viongozi wa madhehebu ya dini ya Kiislamu na Kikristo alipowaita ofisini kwake ili kujenga mahusiano kati yao.
Miseme alisema viongozi wa madhehebu ya dini wapo karibu na jamii,hivyo wanayo  fursa kubwa ya kuweza  kubaini uhalifu na wahalifu
Aidha kamanda huyo wa polisi amewasisitiza viongozi hao kuendelea kufanya doria za kiroho maana wakifanya hivyo uharifu utapungua nchini na  waumini wao watapata  baraka na thwawabu,maana kwa upande wao polisi wanafanya doria za kimwili.
Misime ameongeza kwa kuwataka viongozi hao kuendelea kuhubiri  utii wa sheria bila shuruti kutokana na wao kuwa karibu na wananchi  kwa kuwa maana wakiitii sheria hiyo hata ajali za barabarani ambazo zimekuwa zinasababishwa na uzembe zitapugua
“Mimi ninawaheshimu sana viongozi wa dini kwa sababu wao ndiyo wanachangia utulivu uliopo nchini,na hata mimi ikiwa wataniona na kosa lolote wasisite kuniita na kunionya kama walivyokuwa wakifanya zamani bila kuongopa cheo cha mtu”alisema Misime.
Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi ametoa onyo kwa baadhi ya askari ambao wamekuwa siyo waamni wanaovujisha siri za Polisi ambazo wananchi wamekuwa wakizitoa kuhusu uharifu na waharifu

Misime alisema, kuwa ili kudhibiti tabia hiyo askari watakaobainika watachukuliwa hatua kali  za kinidhamu ikiwemo na kufukuzwa kazi.
Kwa upande wa viongozi wa madhehebu ya dini  wakizungumza baada ya kikao chao kwisha walisema kuwa watahakikisha wanashirikiana na jeshi hilo,
Kaminyoge Andendekisye ambaye ni mchungaji wa kanisa la Moroviani Iringa road alisema mahusiano kati ya jeshi la polisi na upande wao yalikuwa mabovu kutokana na kutotambuliwa kama wana uwezo wa kuweka hali ya utulivu katika jamii.
Kwa  upande wake Usitadhi Musa Jamaa alisema kuwa kitendo cha  jeshi la polisi kukaa nao ni dalili za jeshi hilo kutambua umuhimu wao hali itakayochagiza kuuweka mjini wa Dodoma kuwa ni sehemu ya utulifu na amani kutokana na ushirikiano huo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...