ASKARI
984 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja -- Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja leo amewapandisha Cheo
Jumla ya Askari Magereza 984 kuwa Koplo wa Magereza, kati yao wanaume
ni 845 na wanawake ni 139 baada ya kuhitimu ya kuhitimu Mafunzo ya
Uongozi katika Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya. Akifunga Mafunzo ya
Uongozi wa Daraja la Kwanza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza,
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga
amewapongeza wahitimu hao kwa kufanya vizuri katika masomo Yao na hivyo
kustahili kuwa Viongozi katika ngazi ya kwanza(NCO's) katika Jeshi la
Magereza. Amewaasa kuzingatia kikamilifu weledi katika kutekeleza
majukumu yao ya kazi na kuhakikisha Kuwa wanalinda, kutetea pamoja na
kusimamia haki za wafungwa kwa mujibu wa taratibu za Magereza ili
kulinda utu wa Wafungwa pamoja na hadhi ya Jeshi la Magereza.
Wahitimu hao wameshiriki kikamilifu katika Mafunzo ya Nyanja zinazohusu
Utawala na Uendeshaji wa Magereza, Ustawi wa Jamii, Uraia, Afya pamoja
na Mafunzo ya Kijeshi. Pia kwa kuzingatia madhara ya Adui rushwa,
wahitimu hao wamefundishwa kwa kina juu ya madhara yatokanayo na
rushwa, mazingira na vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi. Pia wahitimu hao
wa Kozi Namba 20 ya Uongozi daraja la kwanza wamepongezwa na Mgeni
rasmi, Kamishna Gaston Sanga kwa mchango wao wa hiari kwa kujitolea Tsh.
2,000,000/= kwa ajili ya kuboresha jiko na miundombinu mingine ya
Chuoni hapo. Imetolewa na; INSP. Lucas Mboje, Afisa Habari wa Jeshi
la Magereza.