1. Kuna jambo huwezi ficha: Kuna jambo
hata ukijaribu kulificha, ukweli wake utajulikana tuu hususani kama utakuwa na
mahusiano ya muda mrefu na mtu husika. Jambo hilo ni ukweli kama unampenda kwa dhati mwenza wako au la.
Mpenzi wako akiwa makini atagundua ‘kufeki’ kwako , kutokana na matendo yako
hususani vile unavyojali hisia zake, usikivu wako kwake, heshima yako kwake, na
unavyojali umoja na kudumu kwa uhusiano wenu.
2. Fedha sikuzote itawasumbua: Hata kama
mtajitahidi kupuuzia umuhimu wa fedha katika mahusiano yenu, fedha itabaki kuwa
mhimili mkubwa wa mahusiano yenu. Hata kama nyote mna ingiza kipato kuna
changamoto mtazipata kama vile kupanga kwa pamoja jinsi ya kutumia fedha zenu,
au kujieleza kuhusu matumizi fulani ambayo mwenzi wako atahoji.
3. Kazi ya ziada: Haijalishi una hisia na
makusudio mazuri sana, bila matendo yanayomridhisha mpenzi wako, hautoweza
kujenga furaha ya kweli katika mahusiano yenu. Ni muhimu pia kutambua kwamba
pamoja na kuwa na makusudio na matendo mazuri, inakupasa kutilia mkazo kuwa
matendo yako na makusudio yako yanaaminika kwa mpenzi wako.
4.Kuna mambo hautokaa ujue ukweli wake: Haipendezi
ila ndio uhalisia kuwa pamoja na ukweli kwamba nyie mmeshibana katika mahusiano
yenu, bado kutakuwepo na siri ambazo haitaambiana. Mbaya zaidi katika siri
hizo, inaweza kuwepo siri ya hisia halisi kuhusu upendo wa mpenzi wako kwako,
au upendo wako kwake. Mfano, wapo waliooana lakini mmoja wapo sio kwamba kweli
anampenda mwenzake, ila alitaraji kujenga upendo akiwa kwenye ndoa, na kweli
anapokuwa kwenye ndoa anajikuta amejenga kumjali mpenzi wake, hatimaye
anajikuta ameweza kumpenda moja kwa moja.
5.Makosa haya ni magumu sana kusahaulika:
Kwa kawaida binadamu wengi hukumbuka mabaya kwa urahisi kuliko mazuri
tunayowafanyia. Na katika mahusiano, makosa haya mawili ; kwanza ni ‘ku cheat’
na pili kutokuonyesha mvuto wa kimapenzi kwa mpenzi wako, yanaweza kuwa makosa
ambayo si rahisi kusahaulika, ingawaje mtu atajitahidi kusamehe, na kujaribu
kufanya mahusiano yaende kawaida.