Taarifa hiyo imetolewa wiki hii na Cpwaa ambaye jina lake ni Ilunga Khalifa kwenye kipindi cha The Jump Off cha Times FM.
“Yeyote ambaye anasikiliza sasa hivi, ajue kwamba Parklane tayari imesharudi na tumeshaingia studio na tumeshagonga ngoma karibia mbili na moja wapo itatoka kabla ya mwezi wa Ramadhan, kwahiyo Parklane imerudi na watu wakae tayari kwa ujio mpya wa Parklane, Sumalee na C to the Pwaa,”alisema Cpwaa.
Kundi la Parklane liliwahi kutamba na nyimbo kadhaa ukiwemo Nafasi Nyingine uliorekodiwa kwenye studio za Tabasamu Records za Mombasa.



